May 26, 2016

Bajeti Ya Wizara Ya Maliasili Na Utalii Yapitishwa, Usafirishaji Wa Wanyama Hai Nje Ya Tanzania Wapigwa Marufuku Kwa Miaka 3

Serikali imesimamisha utoaji wa vibali na uuzaji wa wanyama hai kutoka katika hifadhi za Taifa kwenda nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 mpaka hapo itakapotangazwa tena.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametoa agizo hilo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge iliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha  shilingi bilioni 135.7.

Prof. Maghembe ameiagiza Idara ya Wanyamapori ipange na kuweka utaratibu mpya utakaotumika kusimamia biashara hiyo pindi itakaporejeshwa tena baada ya kumalizika kwa muda wa zuio la Serikali la miaka 3 ikizingatia  mazingira ya uhifadhi wa wanyama hao.

USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA NCHI.
Amesema kumekuwa na taarifa za baadhi ya watanzania wasio waaminifu ambao wamekua wakijihusisha na vitendo vya kusafirisha wanyama hai waliokatazwa kinyume cha utaratibu jambo ambalo limeisababishia Serikali ipoteze mapato kutokana na wanyama hao.

Kuhusu wanyama wanaoruhusiwa kusafirishwa kama nyani, Kenge,ndege, kobe, wadudu na tumbili amesema kuwa wamekuwa wakisafirishwa  kinyume na utaratibu na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa ajili ya kutumiwa na makampuni ya kimataifa kwenye shughuli za utafiti wa kisayansi wa tiba na chanjo.

Amesema makampuni hayo yamekuwa yakinufaika binafsi kwa kupata fedha nyingi pindi yanapofanikiwa kupata chanjo au tiba husika huku maeneo waliokotoka yakipata fedha kidogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imeamua kulifanyia kazi.

 UTALII KUSINI MWA TANZANIA NA MAENEO MENGINE.
Amesema Serikali itatekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji wa Utalii wa Kusini ili kuweka mazingira wezeshi na kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikisababisha watalii kushindwa kufika katika maeneo ya hifadhi za Taifa eneo la ukanda wa kusini  mwa Tanzania.

 Baadhi ya maeneo yatakayoshughulikiwa ni gharama ya usafiri wa ndege  kwenda na kurudi katika maeneo hayo kuwa kubwa hadi kufikia Dola za kimarekani 1800 jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa watalii hao.

Amesema Serikali itaanzisha vituo vya kuwekea mafuta ya ndege mahali vilipo vivutio vya utalii ili kuziwezesha ndege ndogo kufika kwa urahisi na kupata huduma ya kuongeza mafuta ili kupunguza gharama kwa wasafiri wanaotembelea hifadhi za eneo hilo.

Aidha amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali itanunua  ndege ndogo abiria ili kuwezeha watalii kufika kwa urahisi katika maeneo ya hifadhiza Taifa.

UTAMBUZI WA MAENEO MAPYA YA UTALII.
Serikali kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya, mikoa na Wabunge itaanzisha mpango mpya kuviorodhesha vivutio vyote vya utalii vilivyo katika maeneo yao ili viweze kutangazwa ipasavyo na kuongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mpango huo itaandaliwa orodha ya vivutio hivyo ili vianzwe kutangazwa rasmi.

Katika kuimarisha shughuli za utalii nchini serikali itaweka mkazo katika uimarishaji wa utalii wa utamaduni, uimarishaji wa maeneo ya historia na Malikale ili kuwezesha eneo hilo kuchangia zaidi katika pato la taifa.

ULINZI NA USALAMA WA HIFADHI ZA TAIFA.
 Prof. Maghembe ameeleza kuwa suala la ulinzi na usalama wa hifadhi zote za Taifa liko kwa mujibu wa sheria na kubainisha kuwa serikali imeanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) litakalochukua mbuga zote zilizokuwa na uongozi ambazo ziko nje ya TANAPA.

 Jeshi hilo litapambana kikamilifu na ujangili, kuimarisha maadili na nidhamu ya askari wa ulinzi wa hifadhi za taifa pamoja na kushughulikia maslahi yao na kuondoa migogoro kati ya askari na wananchi.

Amesisitiza kuwa mara baada ya Bunge la Bajeti, Wizara itakutana na wahifadhi wakuu wote ili kuweka vigezo vya kuzingatia katika majukumu yao na kusisitiza kuwa wahifadhi wote watakaoshindwa kwenda na kasi ya vigezo vilivyowekwa hawatajumuishwa kwenye jeshi hilo.

Aidha, amekemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi kupiga raia na kuchoma nyumba za wananchi kuwa havikubaliki na ni kinyume cha majukumu yao.

” Nimesikiliza kwa makini michango ya wabunge na nimesikia wafanyakazi katika hifadhi zetu wanapiga raia wanaua mifugo na kuchoma nyumba za wananchi jambo ambalo halikubaliki, hatukuwatuma kufanya hivyo” Amesisitiza Prof.Maghembe.

MIGOGORO YA MIPAKA MAENEO YA HIFADHI.
Serikali imesema mpaka sasa kuna migogoro ya ardhi 281, kati ya hiyo 35 ambayo ni sawa na asilimia 12.5 ni migogoro ya hifadhi na kuita  Mikoa yenye migogoro hiyo kuwa ni pamoja na Mara , Tanga na Kagera inachukua jumla ya asilimia 50.

Aidha, amesema kuwa mkoa wa Tabora unaongoza kwa kuwa na eneo kubwa la ardhi na unaongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya hifadhi kwa asilimia 40.

Katika kuishughulikia migogoro hiyo Serikali imeziagiza wizara za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maji na Umwagiliaji, TAMISEMI, Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana pamoja katika kutatua migogoro yote ya ardhi nchini.

UBORESHAJI WA MAENEO YA HIFADHI NA MAMLAKA ZA UHIFADHI.
 Amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 kiasi cha shilingi bilioni 1 kimetengwa kushughulikia usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo vya kisasa  katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro vitakavyokuwa na uwezo wa kugeuza maji taka kuwa poda ili kuweka mazingira yote ya mlima huo kuwa safi.

Aidha,amesema kuwa Mamlaka za hifadhi za Taifa zimeendelea kuchangia katika maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, miundombinu ya barabara, utoaji wa madawati katika halmashauri mbalimbali nchini.



Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger