Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(Wa kwanza kushoto) akikaribishwa eneo la Hospitali na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimana(Wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Mkurugenzi wa MOI ambaye ndio mratibu wa kambi tiba ya GSM DK Othman KIloloma(Wa nne kutoka kushoto) na Meneja wa Taasisi ya GSM BI Shannon Kiwamba( wa pili kutoka kushoto)
Kambi hiyo kwa sasa ipo Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya Mwanza, Singida, na Shinyanga.
Akieleza sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho kumaliza awamu ya kwanza, Mheshimiwa Mavunde amebainisha kwamba kwanza, ni kwa sababu alisikia kambi iko katika jimbo lake, lakini jingine kubwa na la msingi likawa ni kupeleka shukrani zake kwa Maafisa wa Taasisi ya GSM wanaoambatana na madaktari kuweka kambi tiba hizo katika kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi kila mwaka.
“Nimeshtushwa na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo, hongereni sana”, alisema Mavunde.
Mavunde amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao, na wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui, kwa sababu moja tu kubwa na ya msingi ya utanzania.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:



0 [disqus]:
Post a Comment