Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Aje’, ameonyesha kuguswa na tatizo hilo ambalo limekuwa likiwasababishia watoto ulemavu wa kudumu.
“Nimeguswa sana na kampeni ya GSM Foundationt katika kuwasaidia watoto wetu wa Kitanzania wanaosumbuliwa na magonjwa ya kichwa kikubwa na mgongo wazi. Toka wameanza shughuli hii, mamia ya watoto wameokolewa kutokana na taabu walizokuwa wanazipata,” aliandika AliKiba kupitia instagram yake.
Aliongeza, “Nimefurahi kutoa japo kidogo katika niliichojaaliwa kuunga mkono kampeni hizi.Nawasihi jamii yenye uwezo kila mmoja kwa nafasi yake kutoa kidogo ili kuokoa maisha ya watanzania.#SupportedByKiba #KingKiba,”
Kwa upande wa taasisi hiyo, wametoa ujumbe wa shukrani kwa msanii huyo kwa kuguswa na jitihada za taasisi hiyo za kusaidia watoto aliokatika wakati mgumu.
“AliKiba tunashukuru sana, kwanza kwa kututembelea katika ofisi yetu ya #GSMFoundation na pili kwa mchango wako uliotupatia wa kiasi cha shilingi milioni ishirini na moja (21,000,000) ukiwa ni mchango wako na kuunga mkono juhudi zetu za kuwafanyia upasuaji watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya kichwa kikubwa na mgongo wazi. Mwenyezi Mungu akujalie kwa moyo wako na kukubariki katika kila unalolifanya,” uliandika ukurasa wa instagram wa taasisi hiyo.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:



0 [disqus]:
Post a Comment