Aug 17, 2016

Hatua za Jinsi ya Kuanzisha Kampuni yako Hizi Hapa

NI ukweli usiofichika kuwa  biashara  na ujasirimali  kwa pamoja vimekua kwa kiwango kikubwa hapa nchini. Yote hii inatokana na sababu nyingi, ikiwemo ya kukua kwa biashara za kimataifa, maendeleo ya mawasiliano, marekebisho ya baadhi ya sera za nchi na sababu nyinginezo.

Kwa hakika hali yote hiyo, imesababisha ugumu kwa wajasiriamali wanaofanya biashara zao nje ya kampuni. Kwa dunia ilivyo kwa sasa, si rahisi mtu kufanikiwa katika biashara yake kama biashara yake hiyo haiku katika mfumo wa kampuni. Hata iwe ndogo ya kuuza mayai au kufuga kuku, mafanikio zaidi ni pale biashara hiyo utakapoifanya iwe katika mfumo wa kampuni.

Ni kutokana na umuhimu huo, imenilazimu niwasilishe mjadala huu kwa wasomaji wangu, hasa vijana, kuhusu kampuni, tukijielekeza zaidi katika aina na uundwaji wake kutokana na Sheria ya Makampuni  ya mwaka 2002.

Kampuni ni nini? 
Awali ya yote, yatupasa tufahamu maana ya kampuni. Kwa ufupi, tunasema kampuni ni muunganiko wa kibiashara wa mtu zaidi ya mmoja ulioundwa na kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni  ya 2002. Katika maana hii, tunaona kwamba kampuni lazima uwe muunganiko wa watu. Waweza kuwa wawili, watatu na kuendelea. Hii ina maana kwamba hakuna kampuni ya mtu mmoja.

Lazima umiliki wake uwe zaidi ya mmoja, uwe na mke wako au mume wako au na rafiki, au na mtoto wako, itategemea mazingira ya biashara yenyewe, lakini huwezi kuwa mmoja.

Pili; tumeona katika maana hiyo kwamba ili iitwe kampuni, lazima iwe imesajiliwa chini ya sheria ya makampuni. Hiyo ndiyo kampuni, zaidi ya hapo biashara yako itakuwa katika mfumo mwingine kabisa, ni kitu kingine na si kampuni.

Aina za kampuni
Kabla hatujaingia katika mchakato wa kuunda kampuni, ni vyema pia tukafahamu aina za kampuni. Hii itakusaidia kujua sifa za kila kampuni na aina ya kampuni unayotaka kuiunda.

Kampuni zimegawanyika katika makundi yafuatayo:-

Kampuni ya umma (public company)
Hii ni kampuni umma kama jina lake lilivyo kwa sababu kwamba kila mtu au kila mwanajamii, anaruhusiwa kuomba  uanachama ikiwa tu atatimiza masharti ya kuwa mwanachama au mshirika. Uanachama katika kampuni ndiyo umiliki. Ukisikia mtu ni mwanachama ( member) ni mmiliki. Na umiliki au uanachama unatofautiana kutokana na kiasi cha hisa anazomiliki mtu.

Kwa hiyoi, katika kampumi ya aina hiyo mtu hawezi kuzuiwa kuwa mmoja wa wamiliki, bali yeyote mwenye uwezo, hata kama ni adui yako, ili-mradi umesajili kampuni kama ya umma, atakuwa pamoja nawe katika umiliki wa kampuni.

Pili; ili kampuni ya umma iweze kuanzishwa ni lazima iwe na wanachama wasiopungua saba. Wanachama wakiwa sita, watano na kushuka chini hawawezi kuanzisha kampuni ya aina hiyo.

Tatu; Wakurugenzi wake lazima waanzie wawili. Maana yake ni kwamba mtu mmoja hawezi kuwa mkurugenzi katika kampuni yoyote ya umma.

Nne; ni kwamba katika kampuni ya umma hisa zake ni huru, ikiwa na maana kuwa hisa zake zinaweza kuhama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Mwanachama mmoja anaweza kumuuzia  mwanachama mwingine hisa zake zote au kiasi. Kila mtu yuko huru na hisa zake, anaweza kumuuzia mwingine au akampa zawadi, haizuiwi.


Kampuni binafsi (private company)
Hii ni aina ya kampuni wengi wetu wameziunda. Karibu asilimia kubwa ya kampuni tunazoziona zikifanya biashara, ni kampuni binafsi. Kampuni hizi zina sifa zifuatazo:-
 
Kwanza; wanachama wake hawazidi 50, bila kuhesabu au kujumuisha wafanyakazi. Pili; hisa zake hazihamishiki kirahisi, kwa maana kwamba huwezi kuuza au kugawa hisa zako kwa mtu mwingine bila ridhaa ya wanachama wenzako.

Kwa kuwa ni kampuni binafsi, mtu yeyote anayeingia lazima awe  amekubalika kwa wanachama wengine, pengine asiwe adui au yeyote asiyehitajika.

Tatu; inakatazwa kwa kampuni binafsi kuwaalika au kuwaita watu wengine wa nje kununua hisa. Nne; inawezekana ikawa hata na mkurugenzi mmoja, na si lazima wawe wawili au zaidi.

Kampuni za kisheria (statutory company).
 Hizi ni kampuni zinazoanzishwa kwa Sheria Maalum za Bunge. Mara nyingi kampuni hizi, huundwa ili kutimiza majukumu maalum katika jamii hasa huduma za kijamii. Taasisi nyingi za Serikali pamoja na mashirika ya umma, huwa ni kampuni za aina hii. Kwa uchache, hizo ndizo aina ya kampuni.


Jinsi ya kuunda kampuni
Huu ndio mzizi wa mada hii kwa kuwa wengi wetu tungependa kufahamu ni taratibu zipi, zinaweza kufanya kampuni ikaundwa. Kwa Tanzania, kampuni inaundwa kwa kufuata utaratibu huu.

Hatua ya kwanza ni kuchagua jina la kampuni. Kampuni lazima iwe na jina linalotambulika na linalojitofautisha na majina ya makampuni mengine nchini.


Hatua hii, kwa lugha ya biashara huitwa ‘Name Search’ ambapo unatakikwa kuandika barua kwa Msajili wa Kampuni, kwa maana ya Brela. Ukifika katika ofisi hizo, utaeleza jina la kampuni linalopendekezwa, hivyo jina hilo huingizwa kwenye mtandao wa makampuni yaliyosajiliwa na Brela, ili kuona kama kuna yenye jina linalofanana na hilo lako.

Kwa kuwa majina yote ya kampuni nchini yako ofisi hiyo, hivyo si rahisi kampuni zaidi ya moja kuwa na majina yanayofanana. Ikibainika kuwepo kwa kampuni yenye jina kama la kwako, Ofisa wa Brela, atakuelekeza utafute jina jingine, na kama atakuta hakuna jina la kampuni linalofanana na la kwako, basi jina hilo litapokelewa kwa hatua inayofuata.

Baada ya jina kuwa limethibitishwa, kwa maana ya kukubaliwa na Msajili wa Kampuni, hatua inayofuata ni kuwasilisha kwa Msajili waraka wa kampuni na katiba ya kampuni.

Waraka wa kampuni au kwa lugha ya kigeni ‘memorandum of association’, ni waraka maalum uliosainiwa na wanachama wote ambao hueleza na kuchambua kile ambacho kampuni itakifanya. Shughuli za kampuni zinatakiwa kuelezwa vyema ndani ya waraka huu. Waraka huu lazima uwe na mhuri wa mwanasheria.

Katiba ya kampuni au kwa lugha ya kigeni, ‘article of association’ kwa upande mwingine, nayo lazima iwe imesainiwa na wanachama wa kampuni husika. Katiba hii ndiyo inayoeleza uendesahaji mzima wa kampuni.

Aidha, inaeleza haki na wajibu wa wanahisa, uongozi wa kampuni, mgao wa mapato, nguvu na mamlaka ya wakurugenzi, mikutano na utaratibu wake, umiliki na ugawaji wa hisa, uhamisho wa hisa na kadhalika. Hii nayo lazima iwe imesainiwa na mwanasheria.

Lazima kupeleka kwa Msajili wa Makampuni maelezo (statement) yanayowahusu wakurugenzi wa kampuni. Maelezo hayo lazima yaambatane na wasifu wa kila mkurugenzi na unatakiwa kuwa umeelezwa vyema.

Lazima pia ijazwe fomu maaalum yenye maelezo yanayohusu anuani kamili ya ofisi za kampuni. Anuani hapa si tu Sanduku la Posta, bali pia mahali zilipo ofisi za kampuni, kwa maana ya mahali ambapo kampuni hiyo itaendeshea shughuli zake.

Aidha, lazima ijazwe fomu maalum ambayo ipo kama kiapo kuonesha kuwa matakwa yote ya kisheria yametimizwa, hivyo kampuni inatakiwa kupatiwa usajili.

Fomu hiyo inajazwa na Wakili au mtu yeyote ambaye jina lake limetajwa katika katiba kama mkurugenzi wa kampuni au katibu wa kampuni. Fomu hii inakuwa ni ushahidi kuwa matakwa yote yametimizwa kwa ukamilifu.

Baada ya kutimiza matakwa yoter hayo, hapo kampuni inaweza kusajiliwa kwa kupewa Cheti cha Usajili. Taratibu zote hizi, ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba, fomu na waraka, mara nyingi na kwa wepesi zaidi, zinashauriwa zifanyike katika ofisi za wanasheria.  

Kwa kumalizia nishauri kuwa kufanya biashara kwa mfumo wa kampuni, ni muhimu mno kuliko ambavyo baadhi ya watu wanaweza kufikiria.

Karibu biashara zote za kisasa, hufanyika kwa mfumo huo wa kampuni. Asikudanganye mtu kuwa atapatikana mfanyabiashara mkubwa kutoka Ulaya, Amerika au hata hapa kwete ambaye atakubali kufanya biashara na mtu binafsi. Labda biashara hiyo iwe ya kukufanya wewe kuwa kibarua!

Kampuni zote za ndani na nje, huwa hazifanyi biashara na watu binafsi, bali kama kama watu hao wamejiunga pamoja na kuwa kampuni.

Nieleweke vyema hapa kwamba ninaposema biashara, simaanishi biashara kubwa sana, bali biashara hiyo hiyo ndogo unayoifanya, hata kama ni ya ufugaji kuku wa mayai au wa nyama, biashara ya kuuza maziwa biashara ya duka la vyakula, biashara ya huduma ya pesa kwa njia ya simu, kuuza mazao, kijiwe chako cha ufundi magari au seremala na kadhalika, zote hizo usizifanye wewe kama wewe.

Ukweli ni kwamba hakuna atakayekupa kazi ya maana kama wewe ni mtu binafsi. Biashara ya sasa haifanywi hivyo. Usikwamishe kukua kwa biashara zako, anza sasa kuunda kampuni yako!

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

1 comment:

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger