Inadaiwa kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu akishirikiana na wenzake amekuwa akifanya shughuli hiyo ya uhalifu, ndipo zilipatikana taarifa za kiintelejensia kuhusiana na uhalifu huo, ndipo askari waliweza kufuatilia na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo.
Aidha kwa sasa jeshi la polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. Aidha jitihada za kuwasaka wenzake wanaodaiwa kushirikiana na mtuhumiwa huyu katika uhalifu huo bado zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza, akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na wahalifu wa aina kama hii, ili waweze kufikshwa katika vyombo vya sheria, kwani jeshi la polisi linaamini endapo wananchi wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lao, tutaweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.
imetolewa na:
DCP: Ahmed Msangi
Kamanda wa polisi (m) Mwanza
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:



0 [disqus]:
Post a Comment