May 19, 2016

Askari JWTZ mwenye asili ya Rwanda atoroka jeshini!

OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.

Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.

Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Hatua ya kutoweka kwa ofisa huyo wa juu wa JWTZ anayetajwa kwa jina moja la Selumbo, imekuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa msuguano wa kauli baina ya Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Kigali.

Chanzo cha msigano huo wa maneno uliogeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia, ni ushauri uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Paul Kagame wa kumtaka awe tayari kukaa meza moja na waasi wa kundi la FDLR wanaopigana Rwanda, kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tayari msigano huo wa Kikwete na Kagame umeanza kutajwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa tishio kubwa la kwanza la ustawi, uimara na misingi ya mshikamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo mataifa hayo mawili ni wanachama wake.

Siku chache baada ya ushauri huo, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete, hata kufikia hatua ya kutoa kauli zenye mwelekeo wa vitisho dhidi yake.

Kauli hizo za Kagame zilisababisha Rais Kikwete, kupitia katika hotuba yake ya mwishoni mwa Julai, kujibu mashambulizi, huku akieleza bayana kushangazwa na kushtushwa na kejeli na matusi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.

Akitumia maneno ya kidiplomasia ambayo yametafsiriwa na baadhi wa wachambuzi wa masuala ya diplomasia na sayansi ya siasa kuwa yanabeba ujumbe mzito, Rais Kikwete alisema alikuwa amesikia yote yanayosemwa kutoka Rwanda na alikuwa hakusudii kuyapuuza.

Kauli hiyo ya Kikwete ambayo ilitanguliwa na ile aliyoitoa siku chache mkoani Kagera ya kuwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini, ilifuatiwa na matukio ya kuondoka nchini kwa Wanyarwanda wanaokadiriwa kuzidi 5,000.

Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya mashaka na kutoaminiana kati ya Tanzania na Rwanda, katikati ya wiki hii, gazeti dada la MTANZANIA Jumatano, lilikuwa na habari kubwa yenye kichwa cha habari kisemacho; ;Nini kinamtia Jeuri Kagame?' ambayo pamoja na mambo mengine, ilieleza namna watu wenye asili ya Rwanda walivyojipenyeza katika taasisi mbalimbali nyeti za umma.

Kuvuja kwa taarifa za kurejea Rwanda kwa maelfu ya wahamiaji haramu sambamba na hizi za sasa za kutoweka kwa ofisa wa juu wa JWTZ kunathibitisha kuhusu kuwapo kwa mwelekeo huo wa mambo.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vinamtaja ofisa huyo kuwa ni mmoja wa makachero wenye asili ya Rwanda waliokuwa wakifanya kazi ndani ya JWTZ na ambao wanahofiwa kuwa watu wenye mawasiliano ya karibu na serikali ya Rwanda, kwa malengo ambayo bado hayajawekwa bayana.

"Ni kweli, huyo ofisa ametoweka jeshini na sijui sababu zilizo nyuma yake;hili suala la kuwa anakusanya taarifa za siri za jeshi letu na kuzipeleka Rwanda nadhani ziligunduliwa na watu wetu ambao wapo kwenye mfumo wa kijeshi," alidokeza mmoja wa watoa taarifa wa MTANZANIA Jumapili.

Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alishindwa kukubali au kukataa, kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo ni zito hivyo alikuwa akipaswa kuzungumza kwanza na viongozi wake kabla ya kulitolea taarifa.

Meja Komba alieleza kuwa, wanajeshi wanaotoroka ni wengi na wapo waliofungwa kwa kosa hilo la utoro.

"Jamani suala hili ni zito, naliogopa, nyinyi hamlioni kama ni zito? Sio kwamba sipendi wananchi wapate habari, suala hili tupeni muda kwanza tulifanyie ;analysis', mbona wanajeshi wengi wanatoroka na hamripoti! Waliotoroka ni wengi, wangine wametorokea Rwanda na kwingine na wamefungwa.

"Ni lazima kwanza niongee na mabosi wangu ndiyo nizungumzie vizuri hili; njoo ofisini Jumatatu (Kesho)," alisema Meja Komba.

Sanjari na tukio hilo, taarifa zaidi zilizonaswa na gazeti hili zimedai kuwa sasa imebainika pasipo shaka kuhusu kuwapo kwa makachero wa Serikali ya Kigali wanaodaiwa kupandikizwa katika taasisi na idara nyeti za serikali kwa ajili ya kufanya ushushu kwa maslahi ya Rwanda.

Inadaiwa kuwa intelijensia ya JWTZ iliyo na mizizi ndani na nje ya nchi ilibaini mapema kuwapo kwa majasusi wa Kinyarwanda ndani ya mfumo wa dola na nyendo zao zimekuwa zikichunguzwa kwa muda mrefu na zilibainisha hali hiyo.

- Source: Mtanzania

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger