Hivi mmegundua nini kwenye siasa za bungeni kwa sasa?? Tushukuru Mungu Bunge halionyeshwi Live upinzani ungetunyoosha hasa.
Nani amesikiliza speech za wabunge wa upinzani ?? Sikiliza speech ya Lema, Sikiliza Speech ya Zito , Sikiliza Speech ya Bulaya na Mdee , sikiliza speech ya Lissu nk zina content na context ya kutosha. Ukiisikiliza unagundua watu hawa walifanya research ya kutosha kabla ya kuja kuongea.
Wamekuna na style nyingine kabisa lakini speech za wabunge wa CCM za kutaka sanamu la Diamond au kuwa na uchungu wa kulia kisa hutaki bunge lionyeshwe live hazitaweza kuwanyima Upinzani kutamba ndani ya Bunge.
Nakishauri chama changu haya:;
1. Wabunge wetu wapatiwe frequent trainings juu ya namna ya kuchangia, namna ya kuandaa hoja, public speaking, and etc.
2. Wabunge wetu wakubali kuingia gharama kuwa na vijana ambao watawasaidia kuwaandalia material za kuzungumza bungeni katika kila mada,hoja, au nafasi wanayotaka kuchangia. Hii itasaidia kuwafanya wapate mawazo mbadala, kuliko wao kudhani they can execute everything at par.
3. Chama kiandae utaratibu wa kuwandaa wabunge wetu kuchangia kuendana na hoja au hotuba fulani.Mfano, kundi fulani lenyewe lichangie hotuba ya wizara ya habari,utalii,elimu na kundi jingine lichangie wizara ya viwanda,fedha,miundombinu,wengine wachangie katiba na sheria, ulinzi etc. Kuwepo na division of specialised parliamentarians. Mbunge huwezi kuchangia kila na kujua kila kitu cha kila wizara.
4. Chama kiandae utaratibu wa kuwa morning briefings kuwapatia wabunge kupitia emails, whatsapp msg etc. Mbunge ajue nini kinaendelea duniani na hata ndani ya Tanzania kabla hajaingia bungeni. Na ikiwezekana wabunge wetu wapate scopes as on Military Intelligence said, wawe ahead of information. Haiwezekani wapinzani wanajua taarifa za ndani CCM tumelala. They need to be like cubs with hunger of strong desire of informations.
5. Lazima kuwepo na utaratibu wa kufanya evening postmortem kwa wabunge tu na sio Waziri, either iwe kila siku jioni au after every two days, wakae kufanya SWOT analysis nani kakosea, nini kifanyike kesho na planning of the week. Ili kuondoa uvuvaji wa taarifa, hizi postmortem zifanyike kikanda au kimikoa. Mnaweza kujiandaa kesho tunaenda kumsema sana Kitwanga kisiasa zaidi ili kuondoa notion sisi hatuisemi serikali.
Nahisi Chadema wanafanya haya hapa juu .......... Kwa aina hii ya wabunge tuliyonayo kama hawatasaidiwa kiuwezo mawaziri wetu watapata shida sana ya kusulubishwa na wapinzani.
Hawa wapinzani ukisikiliza hoja zao huachi kurudia kuisikiliza tena. Hatuwezi kwenda kwa kutetea bangi iuzwe kihalali, hatuwezi kwenda kwa kulia kisa watu wanataka bunge live, Hatuwezi kwenda kwa kudai sanamu ya Diamond.
Hatuwezi kwenda kwa mawaziri kila saa kupiga picha na kuzisambaza mitandaoni. Tunataka mkiandika huku mitandaoni mje na hoja zinazojibu matatizo ya wananchi si kila saa kusema leo nilikuwa hapa mara kesho pale. Andiken namna ya kufufua viwanda, namna ya kuwapatia ajira vijana, namna ya kufufua kilimo chetu nk.
KWELI ITATUWEKA HURU.
Ole Mushi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment