Shukrani za pekee zinaenda kwa mshambuliaji wa Burundi Amis Tambwe kwa magoli yake mawili yaliyoisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Tambwe aliiandikia Yanga bao la kwanza dakika za mwanzo kipindi cha kwanza ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Dakika ya 47 kipindi cha pili, Tambwe aliifungia Yanga bao la pili lakini dakika moja baadaye Didier Kavumbagu aliirejesha Azam kwenye mchezo baada ya kuifungia bao ambalo ndiyo lilikuwa la kufutia machozi.
Wakati Azam wakipambana kusawazisha goli, Deus Kaseke alizima ndoto za Azam baada ya kufunga bao la tatu na kuihakikishia Yanga ubingwa wa FA.
Ubingwa huo unakuwa ni wa tatu kwa Yanga kwa mashindano ya ndani ambayo yanasimamiwa na TFF, Yanga ilianza kwa kutwaa Ngao ya Jamii mapema kwezi August mwaka jana kwa kuifunga Azam, kisha wakatwaa taji la VPL kabla ya kumaliza na FA Cup.
Ubingwa wa FA Cup unaipa Yanga kiasi cha shilingi milioni 50 za kitanzania ambazo zimetolewa na mdhamini wa mashindano hayo ambaye ni Azam Media.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment