Katika marekebisho ya Sheria ya Elimu, Sura ya 353, Serikali inapendekeza kuanzisha zuio la kuoa au kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari na atakayetiwa hatiani, atafungwa miaka 30 gerezani.
Wabunge waliochangia muswada huo walieleza kuwa maboresho hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya wanafunzi kupachikwa mimba na wanaume, maarufu kwa jina la mafataki, ambao huishia kulipa faini ya Sh500,000 au kifungo kidogo cha miaka mitatu kwa kosa la pili, adhabu waliyodai ni ndogo.
Hata hivyo, uliibuka wasiwasi kuwa huenda baadhi ya watu wakafungwa kwa kubambikiziwa ujauzito, hivyo kupendekeza katika ushahidi wa suala hilo, vipimo vya vinasaba (DNA) vitumike kabla na baada ya watoto kuzaliwa ili kuthibitisha iwapo aliyefungwa ni baba wa mtoto.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment