Jul 15, 2016

Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara Ya Afya Kuhusu Uvumi Unaosambazwa Katika Mitandao ya Kijamii

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na Uvumi katika Mitandao ya Kijamii kuwa Serikali imeamua kushusha Mishahara ya Madaktari kwa asilimia 30% ili kuendana na dhana ya Hapa kazi tu na kuwa Serikali   imekusudia kufuta malipo ya Posho za Wataalamu wa Afya walio katika Mafunzo kwa Vitendo .Ufafanuzi kwa Umma wa Watanzania na Watumishi wa Sekta ya Afya ni kuwa taarifa hizo siyo za kweli.

Taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu (Afya) alipokuwa anaongea na Watumishi wa  Hospitali ya Bugando  ililenga kutoa ufafanuzi kwa Watumishi wa Hospitali hiyo kuhusu kufutwa kwa kibali cha Msajili wa Hazina kilichowawezesha  watumishi wa Hospitali hiyo kulipwa Mishahara ya Taasisi zilizo chini ya Msajili wa Hazina tangu mwaka 2012.

Uamuzi huo wa Msajili wa Hazina unatokana na ukweli kwamba Hospitali ya Bugando siyo Shirika la Umma na hivyo wanastahili kulipwa mishahara sawa na watumishi wengine wa Serikali Kuu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kati ya Serikali na Baraza  la Maaskofu Tanzania  (TEC) ambao ndio wamiliki wa Hospitali ya Bugando.

Aidha, ieleweke kuwa mishahara ya Watumishi wa Sekta ya Afya haizingatii ngazi ya Vituo vya kutolea huduma kama vile Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali, au Hospitali za Rufaa bali huzingatia uzito wa kazi na majukumu ya kada husika. Hivyo, mshahara wa Daktari wa Hospitali ya Wilaya ni sawa na ule wa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda.

Kutokana na maelezo haya, uamuzi huo wa Msajili wa Hazina utaihusu Hospitali ya Bugando pekee na siyo Hospitali zote za Kanda kwa kuwa dosari hiyo haikutokea katika Hospitali nyingine za Kanda.

Kuhusu ajira mpya kwa mwaka 2015/2016 ufafanuzi ulitolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba hakutakuwa na ajira mpya hadi hapo Zoezi la Uhakiki wa Watumishi Serikalini litakapokamilika.  Hivyo, vibali vya ajira vilivyokuwa vimetolewa vimefutwa hadi hapo itakapotamkwa vinginevyo.

Kadhalika, kumekuwa na Uvumi kuwa Serikali inakusudia kufuta posho ya ‘Interns' kuanzia mwaka huu wa fedha.  Taarifa hii pia siyo sahihi kwa kuwa hakuna chombo chochote cha Serikali ambacho kimetoa maamuzi hayo.

Wizara inasisitiza kuwa maamuzi ya Serikali hutolewa na Mamlaka husika  kwa nyaraka. Hivyo, watumishi wa Sekta ya Afya na wananchi kwa ujumla wanaaswa kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka za Serikali kuhusu Masuala yanayowahusu ambayo mara nyingi hutolewa kwa nyaraka badala ya Mitandao ya kijamii,

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Afya
14 Julai, 2016



Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger