Aug 2, 2016

Kuhamia Dodoma Kunahitaji Tathmini ya Kina

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kuwa kabla ya mwaka 2020 wizara, idara na taasisi zote za serikali zinapaswa kuhamia Dodoma.

Hata hivyo mpango huo umeharakishwa zaidi baada ya Waziri Mkuu kutangaza kuhamia Dodoma kabla ya mwezi September mwaka huu na kuagiza wizara zote kufanya hivyo mwaka huu. Agizo hilo limeanza kutekelezwa kwa baadhi ya wizara kuanza mchakato wa kuhamia Dodoma kwa kuhamisha naadhi ya idara zake.

Wizara ya Elimu ni moja ya wizara zilizoitikia wito huo kwa haraka. Kwa mujibu wa Dokezo lililotolewa na wizara hiyo idara tano zitahamia Dodoma kabla ya tarehe 15 mwezi August na idara zilizosalia zitahamia kabla ya mwezi September.

Kwanza nipongeze nia ya Rais Magufuli za kufanya Dodoma kuwa makao makuu ya serikali na mji mkuu wa nchi. Ukweli ni kwamba Dodoma ilikua mji mkuu kwa jina tu lakini mji mkuu kiutendaji ulikua bado ni Dar es Salaam. Kwa miaka mingi historia ilipotoshwa kuwa mji mkuu ni Dodoma lakini ukweli ni kwamba mji mkuu ulikua ni Dar es Salaam.

Huwezi kusema Dodoma ni mji mkuu wakati wizara zote, idara zote na makao makuu ya taasisi zote kubwa yapo Dar es salaam. Kitu pekee kilichokuwepo Dodoma ni bunge, lakini uwepo wa bunge mjini Dodoma haukuweza kuifanya iwe mji mkuu wala makao makuu ya serikali kwa sababu bunge si sehemu ya serikali. Kwahiyo nimpongeze Rais Magufuli kwa kuamua kutekeleza kwa vitendo mpango huo.

CHANZO CHA MPANGO WA KUHAMIA DODOMA

Wazo la kuhamia Dodoma liliasisisiwa na Mwalimu Nyerere mwanzoni mwa miaka ya 1970. Mwalimu alitaka kuona Dodoma ikistawi na serikali kuweza kuhamia huko ili kutekeleza kwa vitendo dhana ya mji mkuu. Baadhi ya sababu zilizomsukuma Mwalimu Nyerere kuichagua Dodoma ni pamoja na mji huo kuwa katikati ya miji yote Tanzania. Hii ingesaidia kurahisisha huduma miongoni mwa watu walioko maeneo ya pembezoni. Lakini pia zilikuwepo sababu za kiuchumi na za kiusalama.

Ili kutekeleza mpango huo Mwalimu Nyerere alifanya mambo matatu makubwa. Kwanza kutafuta rasilimali (fedha) za kuijenga Dodoma na kuifanya kuwa mji mkuu wenye hadhi, ambapo alifanikiwa kupata ufadhili shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP).

Pili alimtafuta mtaalamu wa mipango miji aliyechora ramani ya mji wa Dodoma Profesa James Stephan Rossaunt, (1928-2009), mhandisi wa Kimarekani mwenye asili ya Kiyahudi. Prof. Rossaunt alifanya kazi yake na kukabidhi kwa Mwalimu Nyerere ramani ya Dodoma kama makao makuu ya nchi.

Baada ya kupokea ramani hiyo Mwalimu Nyerere alianzisha mamlaka ya ustawishaji wa makao makuu (CDA) mwaka 1973 kuipa jukumu la kustawisha Dodoma kuwa mji mkuu kwa kufuata mpango ulioandaliwa na Prof.Rossaunt. CDA ikaanza kutekeleza mpango huo lakini kwa kusuasua. Haikuweza kujenga hata jengo moja la wizara au idara kubwa ya serikali, haikuweza kuratibu ujenzi wa miundombinu, haikuweza kujenga vituo vya huduma za kijamii kuweza kukidhi mahitaji ya mji mkuu. Kwa kifupi CDA haikuweza kukidhi matarajio ya kuifanya Dodoma kuwa mji mkuu.

NINI KILIIKWAMISHA CDA?

Sababu kubwa iliyoifanya CDA kusuasua ni kukosa fedha. Tangu kuanzishwa kwake serikali imekuwa ikitoa fedha kidogo sana kwa CDA hali inayoifanya ishindwe kustawisha Dodoma kuwa mji mkuu.

Kwa serikali ya Mwalimu Nyerere haikua na fedha za kutosha ndio maana akaomba msaada Umoja wa mataifa ambao hata hivyo haukutosheleza mahitaji. Mwalimu hakuwa na rasilimali za kumuwezesha kupata fedha nyingi za kustawisha Dodoma kuwa mji mkuu.

Mwalimu hakuwa anachimba madini, gesi, wala sekta ya utalii haikua na pato kubwa. Kwahiyo mpango wa Mwalimu wa kufanya Dodoma kuwa makao makuu ulikwamishwa kwa kukosa fedha. Mwalimu alikua na nia (willngness) lakini hakua na uwezo (ability).

Katika uchumi ili uweze kuwa na nguvu ya soko (purchasing power) unapaswa kuwa na mambo makubwa mawili. La kwanza ni nia (willingness) na pili ni uwezo (ability). Ukiwa na nia ya kununua gari lakini huna uwezo huwezi kununua. Na ukiwa na uwezo wa kununua gari lakini huna nia huwezi kununua pia. Kwahiyo nia na uwezo vinakwenda pamoja. Ni pande mbili za sarafu moja. Mwalimu Nyerere alikua na nia lakini alikosa uwezo.

Waliomfuata (kabla ya JPM) walikua na uwezo lakini walikosa nia. Baada ya Mwalimu Nyerere pato la taifa limekua likiongezeka mwaka hadi mwaka, rasilimali za ndani kama madini, gesi, utalii, kilimo, vimechangia kukua kwa pato la taifa, pamoja na mikopo na misaada kutoka nje. Kwahiyo serikali zilizofuata baada ya Nyerere zilikua na uwezo lakini hazikua na nia.

JE KUNA FAIDA YOYOTE SERIKALI KUHAMIA DODOMA?

Baadhi ya watu wanauliza kama sababu zilizomfanya Mwalimu Nyerere kutaka makao makuu ya nchi kuwa Dodoma bado zipo hadi leo. Je kuna faida yeyote ya kuhamia Dododa? Majibu ni kwamba zipo faida nyingi sana za serikali kuhamia Dodoma.

Moja ya faida za kuhamia Dodoma ni kutasaidia wakazi wa mikoa ya pembezoni kuweza kupata huduma kirahisi Dodoma kuliko kuzifuata Dar es Salaam. Kwa mfano mwananchi wa Bukoba anayefuatilia kusajili kampuni yake hatalazimika kusafiri tena kwenda Dar es Salaam, badala yake ataishia Dododma.

Pia mji wa Dodoma utakua na kuibua fursa nyingi za kiuchumi. Kwa sasa soko kubwa la bidhaa na chakula lipo jijini Dar es Salaam kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu. Kwahiyo Dodoma kuwa mji mkuu itasaidia kukua kwa ongezeko la watu, na kuibua fursa mpya za kiuchumi. Vilevile itasaidia kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam kwa sababu watumishi wengi wa taasisi za serikali watahamia Dodoma.

Pia itasaidia serikali kupunguza gharama za kuwahudumia watumishi wake wanapoenda Dodoma kikazi hasa kipindi cha bunge. Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwalipia gharama za malazi, chakula na usafiri watumishi wake kama Mawaziri, Makatibu wakuu, Wakurugenzi wa wizara na wakuu wa mashirika mbalimbali wanaokwenda Dodoma kipindi cha bunge. Lakini ikiwa serikali itahamia Dodoma gharama hizo hazitakuwepo kwa sababu watakuwa wakitokea hapohapo Dodoma, na hivyo fedha walizokuwa wakitumia zitaweza kutumika katika mipango mingine ya maendeleo.

Pia faida nyingine ya kuhamia Dodoma ni kuimarisha usalama wa serikali kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Yericko Nyerere cha “Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi”. Kwa mujibu wa kitabu hicho, makao makuu ya serikali nyingi duniani hayapaswi kukaa pwani (cost) bali hukaa ndani (inland). Hata Kenya wana mji uliopo Pwani (Mombasa) lakini makao makuu yapo Nairobi. Afrika Kusini wana miji mingi iliyopo Pwani kama Port Elizabert na Johanesburg lakini mji mkuu ni Pretoria. Hata Marekani vivyohivyo. Hii ni kwa sababu usalama kwa miji iliyopo “inland” ni mkubwa zaidi kuliko miji iliyopo pwani (cost) au mipakani.

JE TANZANIA NI NCHI YA KWANZA KUHAMISHA MAKAO MAKUU YA NCHI?

Daktari Christopher Cyrilo anasema ikitokea, makao makuu yakahamishwa kutoka Dar es salaam yalipo sasa na kuelekea Dodoma, Tanzania itakuwa imeungana na nchi zingine chache katika historia. Nigeria ilihama kutoma Lagos kuelekea Abuja mwaka 1991. Urusi ilihama kutoka St. Peterberg kwenda Moscow mwaka 1918. Pakistan ilitoka Karachi kwenda Islamabad mwaka 1961.

Kazakhstan ilitoka Almaty kwenda Astana mwaka 1997. Brazil ilitoka Rio De Janeiro hadi Brasilia miaka ya1950s. Ivory Coast ilitoka Abidjan na kuhamishiwa Yamoussoukro kwa upendeleo wa Rais Felix Houphoet aliyezaliwa mji huo.Myanmar/Burma ilitoka Rangoon (Yangon) kwenda Naypyidaw mwaka 2005. Belize ilihama kutoka Belize City, na kuhamia Belmopan mwaka 1970.

Kwa hiyo kuhamisha makao makuu ya nchi sio suala la ajabu. Zipo nchi kadhaa zimehama. Pia ni suala lenye faida nyingi za kiuchumi, kijamii na kiusalama. Kwa hiyo nia hii ya Rais Magufuli kuhamia Dododma ni nzuri na imezingatia maslahi ya tyaifa. Lakini je uwezo wa kuhamia Dodoma kwa sasa upo? Rais Magufuli ana nia (willingness) lakini tujiulize je anao uwezo (ability)? Asije akarudia kosa lilelile lililofanywa na Mwalimu Nyerere ambaye na yeye alikuwa na nia lakini akakosa uwezo wa kifedha.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameonesha hofu ya mpango wa Rais Magufuli. Licha ya nia yake nzuri lakini je ana uwezo wa kifedha kutekeleza mpango huo?

Mbunge wa Chadema (Viti Maalumu) Mh.Anatropia Theonest anahoji "Serikali iliwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka huu wa fedha kiasi cha takriban 27 trillion, kikijumlisha mapato ya Ndani, ya nje, Misaada na Mikopo mbalimbali, lakini sikusikia popote mpango au mkakati wa serikali wa kuhamia Dodoma."

Anahoji Anatropia kisha anaendelea "Sipingi serikali kuhamia Dodoma la hasha, napinga kukurupuka kwa serikali kuhamia Dodoma. Ikumbukwe Dodoma ni mji mdogo sana, kipindi cha bunge tu barabara zote mjini hukumbwa na adha ya foleni, nyumba zote za kulala wageni hufurika, na wakati mwingine hata wabunge kukosa maeneo yenye usalama ya kuishi."

Anatropia anashauri "Kuhamia Dodoma ni mchakato unaohitaji fedha. Miundombinu lazima kuandaliwa, ofisi za wizara na idara mbalimbali za serikali lazima kuandaliwa na hata maeneo watakayofikia watumishi.

Ikumbukwe Dodoma ni kati ya Miji yenye zuio la kujenga majengo marefu, kutokana na kuwepo kwenye eneo la bonde la ufa. Hivyo inahitajika ardhi ya kutosha kujenga majengo mengi yatakayoweza kukidhi haja ya kuufanya mji huo kuwa Makao makuu. Je serikali imejipanga? Kipaumbele cha kuhamia Dodoma kilipaswa kuakisiwa katka mkakati wa Mpango wa Maendeleo wa miaka 20, kumi na wa miaka mitano.”

Nae Dk.Joe Mugasa ni miongoni mwa Watanzania wenye hofu juu ya uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma kwa ghafla bila kuwa na mpango wa kisayansi ambao ulipaswa kuakisiwa kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha. Mugasa anahofu serikali kushindwa kutekeleza mpango huu kwa ufanisi kutokana na kushindwa kujipanga. Ametolea mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Dadoma Jordan Rugimbana wa kutaka apewe wiki mbili kwanza ili akamilishe baadhi ya mahitaji muhimu. Lakini je wiki mbili zinatosha kuboresha miundombinu, na kuboresha huduma? Kaili ya mkuu wa mkoa Rugimbana ni kiashiria cha wazi kuwa serikali inahama bila kujipanga.

Aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini Mhe.David Kafulila amehoji "Kwanini wazo la kuhamia Dodoma halimo kwenye ilani ya CCM ambayo Rais Magufuli aliitumia kuombea kura? Kwanini wazo hilo halikuwa moja ya ahadi zake wakati akijinadi? Kwanini halimo kwenye mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka miaka mitano uliopitishwa kabla ya bajeti? Kwanini wazo hilo halimo kwenye bajeti ya serikali ilopitishwa mwezi June?"

Hiki ni kiashiria kwamba si serikali wala si Rais Magufuli aliyekuwa na wazo wala mpango wa kuhamia Dodoma kwa sasa. Serikali haiukujipanga kuhamia Dododma kwa sasa. Kwahiyo wazo hilo limekuja bila kuandaliwa mpango wa utekelezaji. Hii inaweza kufanya mpango huo kushindwa kufanikiwa kwa ufanisi.

NINI KILIPASWA KUFANYIKA?

Baada ya Rais Magufuli kupata wazo hilo alitakiwa kuita wataalamu mbalimbali akae nao na kuwaeleza. Kisha wamshauri kitaalamu namna ya kutekeleza wazo lake kwa ufanisi. Hii ingetoa nafasi ya wazo hilo kuingizwa kwenye mpango wa maendeleo wa muda mrefu na muda mfupi na kuingizwa kwenye bajeti ya nchi. Hii ingempa Rais nafasi ya kutosha kutafuta fedha za kuijenga Dodoma kuwa na hadhi ya mji mkuu.

Lakini pia serikali ingeweza kupitia upya (review) ramani ya mji wa Dodoma kama inahitaji kusukwa upwa kukidhi mahitaji ya mji mkuu. Ramani iliyopo sasa ni ile iliyochorwa na Prof.Rossaunt miaka zaidi ya 40 iliyopita. Je bado ramani ya mji mkuu ya miaka 40 iliyopita inaweza kukidhi mahitaji ya leo?

Wakati mji wa Dodoma unapangwa kuwa makao makuu ya nchi haukuwa na idadi kubwa ya watu kama ilivyo leo. Pia maendeleo ya sayansi na teknolojia hayakuwa kama ilivyo leo. Kwa hiyo ni muhimu kupitia upya ramani ya mji huo na kuifanyia marekebisho makubwa kabla ya kuamua kuhamia rasmi Dodoma.

Imechapwa #JamboLeo Jumanne 02/08/2016, uk.14

Malisa G.J

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

1 comment:

  1. Mwacheni Rais afanye kazi zake na nia yake njema ya kuhamia Dodoma kwani mnaojidai washauri muda wore mlikuwa wapi ndio muibuke sasa kwani hamkujua makao makuu ni Dodoma mbona hamkutoa ushauri kuhusu miundombinu bora mpaka Rais anatangaza kuhamia Dodoma.Mh Raid endelea na nia njema ya kuhamia Dodoma kwani watu wengi wanajua kukosoa kila kitu.

    ReplyDelete

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger