Snura alizungumza haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa licha ya kupata usumbufu huo kwa wanaume hao lakini amekuwa akijitunza na kujiheshimu kwani anafanya hivyo kulinda kazi yake na heshima yake kama mwanamke.
"Unajua watu wakisikia Snura Chura huwa wanatokea wengi sana, na kweli huwa napata shida sana kwa wanaume wengi wenye matamanio, na inawezekana kweli kati yao wapo wenye mapenzi ya kweli na mimi lakini ndiyo hivyo, kitu nachozingatia sana ni kuilinda kazi yangu, hivyo wanapotokea wanaume wa namna hii mimi nachokifanya siku zote ni kuwa mbali nao kabisa ndiyo maana nashinda vishawishi hivyo kila siku" alisema Snura
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment