George Masaju Masaju |
Amesema neno UDIKTETA siyo sahihi kwa kuwa nchini Tanzania hakuna udikteta kwa kuwa serikali inafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria na nchi inaendeshwa kwa kuzingatia mgawanyo wa madaraka wa katika miimili yote mitatu ya dola.“UKUTA lengo lake ni nini, ni sawa na kuwatenganisha wananchi na serikali yao” Amesema Masaju na kuwataka wananchi kutambua kuwa Septemba Mosi ni siku ya Majeshi nchini huku akishangazwa na CHADEMA kuchagua siku hiyo kuzindua kampeni yao aliyodai kuwa ina lengo la kuvuruga nchi.
Masaju amewataka viongozi wa vyamavya siasa nchini kutii mamlaka za dola ikiwemo Jeshi la Polisi na mahakama iliyowapa mwongozo juu ya ombi la kupinga zuio la jeshi la polisi na pia kufuata ushauri waliopewa na Tume yaHaki za Binadamu na Utawala Bora juuya kutokuwepo kwa udikteta nchini.
Amesema sababu kuu za kuzuia Oparesheni ni mbili ambazo ni hali ya usalama kutokuwa shwari, pamoja na kutokuwepo kwa udikteta nchini.
Chanzo : EATV
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment