Aug 18, 2016

Ushauri: Nimechoka na Hii Hali ya Kuachwa na Wanaume

Habari zenu,

Naombeni ushauri wenu ili niepuke na hii hali,

Kama mtu atashindwa kunishauri naomba aache maana sipendi kutukanwa.

Mimi ni binti ni mkazi wa Dar ila kikabila nimetokea mkoa uliopo karibu na Kanda za Ziwa, na mshukuru Mungu kaniumba msichana wa kawaida sina uzuri kama malaika wala sina ubaya ni wakawaida tu, nimepitia maisha ya mahusiano yenye kuniumiza sana, mara ya kwanza nilikuwa na mvulana ambaye ni msukuma wa Shinyanga kipindi nimeanza mahusiano yeye alikuwa chuo nikamvumilia sana mpaka akamaliza chuo.

Mungu akamsaidia akapata kazi katika ofisi moja kubwa tu hapa Dar alikuwa ni mwanasheria, nilijitahidi niwe mwaminifu nikijua atakuwa mume wangu lakini alikuwa ni mtu muongo na kunidanganya sana, nikaja kugundua kumbe aliacha mchumba wake kwao na alikuwa na watoto wawili niliumia sana nikapiga moyo konde nikaanza maisha mapya.

Badae nilipata mtu mwingine alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni moja ya simu kubwa tu hapa Tz huyo kijani alikuwa ni mchagga na mshukuru Mungu katika swala la kunijali alinijali sana yeye alikuwa anasali haya makanisa ya kilokole mimi ninasali Lutheran, kweli tulipendana sana ikafika muda wa kunipeleka kwao ila mama yake mzazi alitokea kunichukia ghafla, hivyo sikuona sababu ya kuendelea nae huku mama yake hanipendi na nikamwambia bora tuachane kuliko kukosa baraka kwa wazazi wako kisa mimi, japo niliumia sana nikamuomba Mungu anipe ujasiri, siku zikaenda nikasahau nikajipa moyo ipo siku.

Baadae nikampata mwanaume mwingine ambaye nilidumu naye zaidi ya miaka minne, kwakweli namshukuru Mungu amenipa moyo wa uvumilivu na sina tabia ya uhuni au tamaa za muda mfupi huyu alikuwa ni msukuma tena wa Mwanza na kiukweli alikuwa kijana mwenye hofu na Mungu sikutegemea kama angenibadilikia baadae, alikuwa anafanya kazi kwenye mgodi mkubwa wa Tz na ndugu zake wengi walikuwa Mwanza hivyo Dar alikuwa anaishi na kaka yake tu hivyo hakuwa mwenyeji sana huku na kama ikitokea kaja Dar likizo basi alikuwa anakuja kwajili yangu, katika kipindi cha mahusiano alipata nafasi ofisini ya kwenda kusoma nje na mawasiliano yetu yalikuwa ni mazuri ilikuwa kila siku lazima anitafute alijitahidi kuniweka karibu nae na kila siku ilikuwa neno lake nitulie akirudi atanioa kwakweli katika hali ya kibinadamu ilihitaji moyo sana lakini nilimshirikisha Mungu kwa kila hatua ili nisiingiwe na tamaa, japo ndugu zangu wengi waliniambia nikipata mtu mwenye nia ya kunioa nisikatae maana hawana uhakika nae lakini nilijitahidi kutowasikiliza.

Badae mawasiliano yalianza kupungua nina weza kumtafuta akawa yupo online anapata SMS lakini hajibu anaweza kujibu SMS badaa ya mwezi ukimuuliza anasema masomo magumu mama, mara naachaga data wazi, nilikuwa naumia sana ila nika note kitu, akapata likizo akarudi wakati namfuata airport nilipomuona nilihisi kabadilika sana, nikajipa moyo labda kutokana na mazingira aliyokutana nayo, likizo ilipoisha aliondoka nikasema ngoja nipime imani yake nikamtumia text kuwa nina mimba sikutegemea, alikuwa mkali chui akani please nitoe mimba sababu siwezi kulea ikiwa baba yake yupo mbali akaniambia usipotoa nakuacha.

Kwakweli niliumia sana nikawaza je ingekuwa ni kweli nina mimba ningekuwa na hali gani, nilichomjibu nikamwambia sawa nitafanya abortion ila usinitafute, badaa ya kama miezi kadhaa alirudi akanitafuta na kuni please turudiane nilikataa nikaamua kuacha nitulize akili na mpaka leo kwenye akili yake anajua nilikuwa na mimba kumbe haikuwa hivyo, katika hali ya kibinadamu nilikaa single karibu mwaka nikapata mvulana huyu amenipita miaka 4 na yeye ni msukuma wa Shinyanga na ni mfanyakazi wa serikalini nilijiona ni mwenye bahati na kikubwa niliona familia yao ni watu wenye hofu na Mungu.

Tulipendana sana na alinijali sana, lakini mwaka huu mwezi wa 4 ndo ilikuwa mwisho wa mahusiano yetu baada ya kunipeleka kwao kunitambulisha ili mwezi wa saba tufunge ndoa, baada ya utambulisho mimi nilirudi Dar sababu mwenzangu kwao ni Dodoma, nilipoondoka kumbe huku nyuma kulikuwa na mtafaruku kati yake na wazazi na kanisa, ni kwamba walikuwa hawataki kijana wao aoe mwanamke anayetoka nje ya kanisa la kilokole, hivyo alianza kubadilika mwenzangu akawa ananiambia ndoa tuhairishe hadi nimalize kujenga nyumba, bla bla zilikuwa nyingi ila nilijua kuna sababu kubwa hataki kuniambia, mwisho wa siku ilibidi aniweke wazi niliumia sana na sikuwaza hata siku moja kama wakristo tuna weza kubaguana kiasi hiki.

Tangu hapo nimekuwa mtu mwenye mawazo mengi, maumivu makali kuna wakati huwa naweza jifungia ndani nalia sana, na pia nimekuwa mtu mwenye hasira kila wakati japo najitahidi ku control hasira, kingine nimekuwa sitamanani mwanaume yoyote yule yani naweza nikaanza mawasiliano na mtu baada ya wiki nampotezea, kubwa nimekuwa na hofu na hawa watu na kikubwa roho ya kupendwa na waume za watu inaniandama na mimi sitaki kabisa kuja kufanya chukizo kwa Mungu ku date na mume wa mtu, wamekuwa wananisumbua sana yani mtu yupo radhi anipe kila ninachokitaka ili mradi anipate, dunia sahivi ina maradhi mengi na mimi sipo tayari nizikwe kwa tamaa, pia nimekuwa muoga na kabila la wasukuma maana ndo nina bahati nao mbaya.

Je nifanye nini ili hii hali isiwepo tena kwenye maisha yangu maana nimechoka kucheza harusi za wenzangu, na mimi natamani siku moja waje wacheze yangu, japo huko kwetu bibi zangu wanasemaga kuna mizimu ya babu zetu inatuandama ndo maana wajukuu tunakuwa hatufanikiwi kwenye malengo tunatakiwa tukafanyiwe matambiko, japo mimi binafsi siamini katika hilo maana namtegemea Mungu.

Naombeni ushauri wenu katika hili, nisameheni kama nitawachosha kwa thread ndefu.

Note: Matusi sitaki.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger