Aug 12, 2016

UVCCM Arusha Wamwomba Dr Magufuli Avunje Jiji

TAMKO LA BARAZA KUU LA UVCCM WILAYA YA ARUSHA MJINI 

1.Tuna mshukuru Mungu ambaye ametukutanisha siku hii ya leo baada kupita kwa uchaguzi mkuu October 2015 pamoja na uchaguzi mdogo wa ubunge na uchaguzi wa serikali za mitaa ambayo ccm ilishinda kwa kiwango chakuridhisha

2.Tunampongeza Dr.John Joseph Pombe Magufuli Kwa ushindi wa kishindo aliyoupata tar 23.7 .2016 pale Dodoma hii ni heshima kubwa kwa ccm na nchi yetu hotuba yako baada ya kuchaguliwa nidira Kwa ccm na kwasehemu kubwa tumeanza kuifanyia kazi

3.Tunampongeza sana Dc wetu wa Arusha mjini ndugu Mrisho Mashaka Gambo kwa kazi mzuri anazozifanya ndani ya wilaya yetu ya kutatua kero za wananchi

katika kutekeleza majukumu yake hayo madiwani wa chadema na mbunge wao wameonyesha kukerwa sana na kero za wananchi kutatuliwa na Dc mfano soko la kilombero lilikuwa limekatiwa maji kwa zaidi ya wiki tatu soko ambalo linahudumia zaidi ya nusu ya wakaazi wa Arusha Dc aliwaamuru AWUSA warudishe maji na maji yanatoka vizur sokoni Kilombero kwanini chadema hawakupendezwa na maji kurudishwa ??je walitaka kipindu pindu kiue watu ili wailaumu serikali ??

jambo lingine ni kata ya muriet ambayo inakabiliwa na kero ya maji umeme na barabara Dc alipowatembelea alikuta wananchi wanachangishwa pesa za kujenga barabara Dc akawachangia lita mia tatu za Dizel pia kuwaita AWUSA nakutoa maelezo kwanini hakuna maji eneo la kwa Mrombo AWUSA walitoa maelezo yao juu yakuwepo kwa eneo ambalo lina maji na huyo mwananchi badala ya kusubiria fidia ya Idara ya maji yeye amekatakata hilo eneo na kuuza Idara yamaji baada ya kukuta hayo ilibidi wazipige X hizo nyumba ili wananchi wengine wasiendelee kujenga eneo hilo jambo la kushangaza badala ya madiwani na mbunge wachadema kuungana na Dc kwenye kazi hiyo mzuri wao walifunga safari wakiwa na mbunge wao lema na meya kwenda kuwadanganya wananchi hao kuwa hawatatoka na wazifute hizo Alama za X

4.Halmashaur ya jiji la Arusha kwa kiwango kikubwa imekosa uadilifu na kuwa kichaka cha siasa chafu na uonevu kwa watu mfano ni suala la maduka ya stand ndogo stand kubwa na soko kuu utaratibu uliyotumika unatia shaka sana yupo mwananchi aliyenyang'anywa duka lake stand ndogo na kupewa mama yake na diwani wa Chadema kata ya unga Ltd yupo mwananchi mwingine aliyenyang'anywa baada ya kuonyesha nia ya kwenda mahakamani aliitwa Halmashaur nakurudishiwa chumba chake alifahamika kwa jina moja la kwayu ambaye nI mjombaake Lema zoezi hili la vizimba halina haki ndani yake naiomba serikali yetu iliingilie kati haki itendeke

pia mh Dc katika kuisimamamia Halmashaur amepinga ufisadi wa madiwani wa chadema kupitisha kujilipa nauli, ya laki moja na elfu ishirini huu niwizi haukubaliki Dc tupo na ww katika kutetea haki za wakaazi wa Arusha lakini pia kwa mbunge wa Arusha na madiwani wake najua hamjavisoma vitabu vya kisheri na katiba ya nchi juu ya majukumu ya Dc kwenye eneo lake la utawala nadhani ni ushamba na umbumbu lema nawenzako someni hapa majukumu ya Dc


Mkuu wa Wilaya:
Uhusiano wa Mkuu wa Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa, upo katika Majukumu ya Mkuu wa Wilaya kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa Na. 7 na 8 (Sura 287) na (Sura 288) (Mamlaka za Wilaya na Miji) na Kifungu Na. 14(3) (a-c) Sheria ya Tawala za Mikoa Na. 19 ya 1997 (Sura 97) kama yafuatayo:-
i. Kuhakikisha kuwa kuna utulivu na amani katika Wilaya;

ii. Kuziwezesha na kuzisaidia Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake kwa kuweka mazingira mazuri ya kuziwezesha Halmashauri kutekeleza kazi na majukumu yao;
iii. Kuhakikisha watu wote na mamlaka zote zinatekeleza maamuzi, miongozo na Kanuni za Serikali mintarafu ukuzaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa;
iv. Kuchunguza uhalali wa matendo au maamuzi ya Serikali za Mitaa zilizo katika Wilaya yake iwapo yametiliwa mashaka na kuchukua hatua ifaayo au kumjulisha Waziri;
v. Kupokea mihtasari ya Halmashauri kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri;
vi. Kumwagiza kimaandishi mtumishi yeyote wa Halmashauri aliye katika vazi rasmi kumkamata mtu anayevunja sheria ndogo ya Halmashauri mbele yake.

UWOZO mwingine kwenye Halmashaur ya jiji la Arusha


Kuhusu Asilimia kumi ambayo tano inakwenda kwa wanawake na tano kwa vijana kwa hapa Halmashaur ya jiji la Arusha inayoongozwa na chadema imakuwa imebubikwa na wizi mkubwa na usiyokuwa na maelekezo mfano kata ya Osunyai kikundi kilichopitishwa ni cha mke wa diwani kata ya Olasite kimepishwa cha mke wa diwani pia madiwani wa chadema wanaoliongozwa jiji la Arusha wameunda vikundi vya mademu zao na mahawara zao hili jambo halikubaliki kabisa

Lakini pia ofisi yangu imepokea malalamiko ya wafanyakazi wa iliyokuwa kampuni ya parking sistem baada ya serikali kuondoa utaratibu wa Tenda Halmashaur ya jiji ilitangaza nafasi za kazi wananchi wa Arusha waliomba lakini walipokaa kwenye vikao vyao vya kamati ya madiwani walikubaliana kila diwani awalete watu watano kutoka kwenye kata yake walifanya hivyo wakati wakitakiwa kusubiria utaratibu wa kuajiri yalikuwepo maelekezo ya serikali kuu kuruhusu Halmashaur zimruhusu wakala aendelee kukusanya jambo la kushangaza Halmashaur ya jiji la Arusha ilikataa kuongeza mkataba kwa wakala ambaye ni ndugu Jastin Nyari kwa vile nikada wa ccm na aligombea ubunge kupitia ccm kutokana na chuki hizi za kisisa Halmashaur imepoteza mapato kwa kiwango kikubwa kipindi chamwanzo alipokuwa anakusanya wakala pamoja na kulipa wafanyakazi na kuendesha huduma zote, alikuwa anailipa Halmashaur kiasi cha tsh.milion sitini ila kwasasa halmashaur kwa inapata hasara kwasababu za hovyo

ushauri wetu:kwasasa kwavile lipo tangazo la Tamisemi la kuruhusu Tenda ndani ya halmashaur siyo sawa jiji letu kuendelea kupoteza mapato kwasababu za hovyo Mkurugenzi aliyepo ambaye nimpya tunaimani naye tunamwagiza afuate taratibu na sheria ya manunuzi Tenda zitangazwe na wapewe watu bila kujali itikadi za kisiasa bali mapato ya halmashaur yetu

8.tunamshauri na kumwomba mh raisi wetu mpendwa aiokoe Arusha kwa kuivunja Halmashaur ya jiji la Arusha maana serikali inapoteza mapato mengi katika jiji letu kwasababu za hovyo

Vijana wa UVCCM wilaya ya Arusha mjini hatutajadili suala la ukuta kwasababu hakuna siku mwkt wa chadema amewahi kutangaza jambo akafanikiwa huu ukuta utaanguka kama ile safari ya mabadiliko ilivyo anguka

SASA NI KAZI TUU KUJENGA CHAMA NA NCHI YETU

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger