Sep 23, 2016

TANESCO Kukata Rufaa Uamuzi Kuilipa Benki Sh Bilioni 311

BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme (Tanesco) imepanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID) ya Uingereza ya kulitaka shirika hilo kuilipa Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) Dola za Marekani milioni 148.4 (Sh bilioni 311).

Fedha hizo ni malimbikizo ya gharama za uwekezaji wa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Independent Power Tanzania (IPTL), Tegeta jijini Dar es Salaam.

Tanesco imesema mpango huo wa kukata rufaa unatokana na kukiukwa kwa sheria na kanuni kadhaa zinazosimamia uendeshaji wa Mahakama hiyo tangu ilipofunguliwa mwaka 2010, ilipotoa uamuzi wa awali mwaka 2014 hadi ilipotoa uamuzi wa mwisho hivi karibuni.

Kutokana na uamuzi huo, Tanesco kwa kumtumia wakili wake Richard Rweyongeza wa Kampuni ya R.K Rweyongeza & Advocate itakata rufaa hiyo ndani ya siku 90 zilizotolewa na Makakama ya ICSID, huku menejimenti yake ikisema ina imani kubwa kwa shirika hilo kupata haki zaidi kuliko ile iliyotolewa hivi karibuni.

Pamoja na uamuzi wa juzi kutokuwa mpya ukilinganisha na ule wa awali uliotolewa na Mahakama hiyo ya Kimataifa Februari 12, 2014, huku ukitoa nafuu zaidi kwa Tanesco, lakini shirika hilo limesisitiza bado yapo maeneo ambayo kama yataangaliwa kwa kina katika rufaa yao yatatoa nafuu zaidi wa uamuzi wa mwisho wa fedha inayopaswa kulipwa, lakini pia mhusika halali wa kulipwa tofauti na ilivyoamriwa.

Akizungumza na jopo la wahariri wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema yapo maeneo ambayo Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo imejiridhisha kuwa yalikuwa na udhaifu wa kisheria na hayakutazamwa vizuri na Mahakama ya ICSID katika kufikia uamuzi wa juzi.

Mramba alisema katika uamuzi wa hivi karibuni, Mahakama hiyo ilishindwa kuzingatia uamuzi wake wa awali wa mwaka 2014, na kutoa maamuzi mapya kama vile kesi hiyo imeendeshwa upya, jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya sheria na kanuni za uendeshaji wa Mahakama hiyo.

Alisema kanuni za Mahakama hiyo zinasema pande zinazoshtakiana zikifungua kesi ya madai katika mahakama hiyo na tuzo kutolewa, pande hizo haziwezi kufungua kesi upya, na kusema kwa vile Mahakama ya ICSID ilishatoa tuzo katika uamuzi wa awali wa 2014, haikupaswa kubatilisha.

Akitolea mfano alisema katika tuzo ya mwaka 2014, pamoja na mambo mengine, Mahakama hiyo ilitoa uamuzi kuwa Kiwango cha Marejesho ya Uwekezaji (IRR) ambacho Tanesco wanapaswa kulipa hakitakuwa asilimia 22.31 wala asilimia 0, lakini cha ajabu katika uamuzi wa karibuni Mahakama hiyo ikabatilisha uamuzi wake wa awali na kuagiza Tanesco kulipa kiwango cha asilimia 22.31.

Awali, akielezea ni kwa nini uamuzi wa hivi karibuni ulitoa nafuu kwa Tanesco tofauti na inavyokuzwa na baadhi ya vyombo vya habari (si HabariLeo), pamoja na nia hiyo ya kukata rufaa, Wakili Rweyongeza alisema katika maombi yake, Benki ya Standard Chartered ilitaka ilipwe zaidi ya Dola za Marekani milioni 300, lakini Mahakama hiyo imeamuru kulipwa kwa Dola za Marekani milioni 148.4, hatua ambayo ni ya ushindi kwa Tanesco.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger