Sep 21, 2016

TATIZO la ATCL Halikuwa Ukosefu wa Ndege..Tusije Tukarudia Matapishi

Na. M. M. Mwanakijiji

Tutafanya makosa makubwa sana na inawezekana tunarudia makosa ambayo tulishawahi kuyafanya kama tutadhania kuwa tatizo la kampuni ya ndege ya Taifa ya ATCL ilikuwa ni kutokuwa na ndege za kutosha au aina ya ndege ilizokuwa nazo. Kudhania kuwa kuleta ndege nyingine mpya za aina yoyote kutatatua tatizo la msingi la kampuni hiyo. 

Kwa mtu ambaye nilishiriki kikamilifu kufichua ufisadi wa ununuzi wa Airbus 320 kwa kushirikiana na wazalendo wengine naweza kusema kuwa kama tunafikiria kuwa ujio wa hizi ndege mpya utatatua tatizo la ATCL tutakuwa tumefanya makosa, au tutakuwa tumerudia makosa. Ikumbukwe kuwa ujio wa ile Airbus 320 nao ulifanywa kwa namna hii watu wakidhania kuwa kuja kwa ndege ile kungelifufua shirika. 

Nina uhakika wengine wameonesha hili na mimi nalirudia tu kwa namna yangu; kwamba tatizo la msingi la kampuni hii - na inaweza taasisi na kampuni nyingine kadhaa serikali ambazo hazijafanya vizuri - kwa kiasi kikubwa ni tatizo la kiuongozi. Nyangenyange wanaporuka angani humfuata kiongozi wao; akiamua kuanza kutua na wao wanatua akiamua kwenda Magharibi na wao wanamfuata. Kanuni hii ipo katika viumbe vingi ambavyo huishi kwa kuwa na kiongozi; tembo, makundi ya simba, fisi hata baadhi ya wadudu huishi kwa kufuata viongozi wao; na wengine hufa wakimfuata kiongozi huyo.

Kampuni ya ATCL kwa muda mrefu imekuwa na shida hiyo ya uongozi; na hapa hatuzungumzii majina au mtu kuwa na qualifications za kisomi; tunazungumzia, maono ya kiuongozi, uthubutu wa maamuzi, usimamizi wa kiutawala, nidhamu ya kazi n.k Kiongozi akiwa dhaifu na akiwa ambaye hana maono yanayopasa ni vigumu sana kuweza kuongoza taasisi ambayo inataka kuingia kwenye ushindani ambapo wapo wengine wakifanya vizuri zaidi. Ni lazima kiongozi awe ni mtu ambaye ni trailblazer kweli kweli. 

Tatizo hili la kiuongozi kwa kiasi kikubwa lilijionesha katika huduma. Na ninaamini kabisa, bila kuboresha huduma hata tuje na ndege zinazotumia warp engine bado tutajikuta tunakosa ushindani. Kama abiria - mteja - anapoanza kununua tiketi hadi hadi anashuka uwanjani hajihisi kuwa amepata huduma inayomstahili kutoka kwenye shirika lake ni vigumu sana kwa abiria huyo kurudi. 

Tusije kutarajia watu wapande ndege za ATCL kwa ajili ya uzalendo; watu wanafuata huduma, unafuu wa bei, heshima na utu ambao unaonekana kuwepo. Nina uhakika tuna watu wanaoweza kutoa huduma ya kisasa, yenye heshima na yenye kuonesha kuwa wanajaliwa wateja kweli kweli. Hawa ndio watu wanaoweza kuvutia abiria kupanda ATCL. Ni lazima watu waone fahari kutumikia kampuni hii na wawafanye watu waone fahari kutumia kampuni hii. 

Ni mpaka pale tutakapoweza kuwafanya watu waone kuwa hii ni kampuni ambayo ina new ethos na ina maadili ambayo yako juu ya kampuni nyingine yeyote ya ndege, basi uwezekano wa kufanikiwa kwa muda mfupi ujao utakuwa mgumu sana kwani hatutaweza kuongeza ndege nyingine. 

Swali ni je, baada ya ujio wa ndege hizo na kuanza kazi watu wataona tofauti katika huduma na katika uongozi? Au tutafikiria kuwa tutaibeba kwa kuwataka watumishi wa umma wanaotaka kusafiri ni 'LAZIMA' watumie ndege yetu hata kama huduma yake si nzuri? 

Hii ni changamoto ya kiungozi. Tusirudie makosa ambayo tulipaswa kujifunza kwayo huko nyuma.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger