Ningekutana na Prof.Lipumba ningemshauri kuachana na Uenyekiti wa CUF kulinda HESHIMA YAKE aliyonayo (Kisiasa na Kielimu) Prof.Lipumba kumbuka watu wanaangalia zaidi Usomi wako kwa sasa kuliko hata kutetea huo UENYEKITI WA CUF. Wewe ni Msomi tena kiwango cha Profesa, unatakiwa ulijue hilo na unasikia kuwa Wewe ni Bingwa wa Masuala ya UCHUMI tena DUNIANI.
Ivi Prof. ni nani?
Ukiwa Prof.maana yake una Digrii Moja, Master, na una Dr. ya elimu! kwa sababu ya kufanya tafiti zenye mashiko katika fani uliyosomea na kwa vigezo ambavyo vimewekwa mwishoni unakuja kutunukiwa Prof. Ukiitwa Prof. Wewe ni mbobezi katika fani hiyo. Na kazi ya Prof.ni kufanya tafiti nyingi ipasavyo na kuandika ili ufanye machapisho kama vitabu na wanafunzi katika vyuo, sekondari au shule ya msingi pamoja na elimu ya awali waje wasome maandiko yako.
Tangu miaka mingi sana huko nyuma, wadadisi wa mambo wanaamini kuwa ukiwa Dr.au Prof. lazima una HEKIMA, BUSARA, NA UTASHI MKUBWA SANA WA KUNG'AMUA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII. Kwa kifupi wewe ni Msomi na msomi yoyote lazima atetee wanyonge. Uwe ni Prof. wa Samaki, Nyuki, Mimea Jamii yote inaamini kuwa lazima wewe umejaa HEKIMA,BUSARA NA UNAWEZA KUNG'AMUA mambo mengi katika Jamii.
Katika Taasisi za elimu zote hasa vyuo vikuu, kama hicho chuo hakina hata Dr. wala Prof.hata mmoja lazima hicho chuo kionekane cha ajabu sana na hakika hakiwezi kupiga hatua nzuri katika kupambana na Dunia katika maswala ya Kielimu. Tena sidhani kama hata kinaweza kuruhusiwa kuanza kutoa elimu ya juu nchi yoyote.
Taasisi za elimu lazima zizingatie vitu vinne,na mitaala yao ijikite katika; Mosi, kuwapa vijana wetu ufahamu wa mambo yatakayowasaidia katika maisha yao na Taifa lao na kuweza kushirikiana vizuri na wenzao; Pili, wapate ujuzi wa kutenda na si kuongea tu kwa yale waliojifunza darasani; Tatu, wajengewe uwezo wa kujiamini kutenda yale waliofundishwa ili waweze kufanya kazi zao kwa ufasaha; Na nne, wajengwe katika nidhamu,kwani nidhamu inasaidia sana katika sehemu nyingi,na isiwe nidhamu ya uoga.
Mwalimu Nyerere alishawahi kunena, ‘’...elimu ni lazima itukomboe kifikira kwelikweli. Inatakiwa kumkomboa mwananchi kutokana na tabia mbaya inayomfanya ayakubali mazingira yanayodhalilisha utu wake kwa kudhani kwamba mazingira hayo ndiyo sitahiki yake”
Haya mambo yote yanategemewa sana yatoke kwa Dr. na Maprofesa wetu nchini.
Mafundisho yanayompa mtu mawazo ya utumwa au unyonge si elimu hata kidogo. Elimu ni lazima iweze kumsaidia mtu kuchambua njia tofauti za kufanya maamuzi na kumfanta aweze kuchagua moja kati ya njia hizo tofauti katika kuhangaikia maisha yake,na lazima impe uwezo wa kutafasiri maamuzi yake kwa vitendo.
Nilirudi kwenye mjadala wenyewe kuhusu Prof.Lipumba. Binafsi nazidi kusisitiza kwa kusema hivi, sawa tufanye Prof.Lipumba anatumiwa kulingana na tuhuma ambazo anapewa na baadhi ya wanachama na viongozi wa chama chake CUF. Swali ambalo najiuliza a unabaki nalo; kwani yeye hawezi kuwaambia wanaomtumia namna ambavyo angependa atumike?!. Nasema hivyo kwa sababu Mimi naamini sana katika kulinda heshima na utu wangu mbele ya umma kuliko jambo lolote lile. Yeye ni Prof.tena sijui kusoma katika vyuo bora kabisa Duniani kwa hiyo anajua kung'amua mambo mengi zaidi na zaidi. Au Jamii inayompinga haimwelewi kwa sababu ya yeye ni Profesa mashuhuri tena mbobezi wa Uchumi??!!
Kwa upande mwingine, inasemekana chama cha CUF hakijafuata utaratibu kulingana na katiba ya CUF ndiyo maana msajili wa vyama vya siasa Dr.Mutungi kaamua kumtambua yeye kama bado ni kiongozi halali wa CUF. Sawa tufanye kuwa CUF walikuwa hawajamjibu barua yake wala kuchukua hatua yoyote ile. Mimi binafsi ningekuwa Prof.Lipumba, hakika ningesoma hata HEWA INAVYOBADILIKA na kujua nifanye hivi kwa ajili ya HESHIMA NA UTU wangu na kubaki Mwanachama wa CUF wa kawaida tu kuliko kuhangaikia Uenyekiti wa CUF wakati najua hata sababu iliyonitoa huko ingali IPO. Nadhani kwa uelewa wangu ningebaki na HESHIMA NA UTU WANGU DAIMA. Lakini sijui maana yeye ni Prof.usikute watu wengi hatumuelewi maana yeye ni mbobezi zaidi.
Ama CUF wamekosea namna ya kumwondoa au wamepatia; Prof.Lipumba amekosa UHALALI wa kuiongoza CUF. Ndiyo maana labda kwa ajili ya elimu yangu ya chini zaidi ya Prof. inawezekana kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kufikiri. Nakumbuka hata Majiniaz kama wakina Isaack Newton, Galileo Galilei, Albert Enstein nao jamii haikuwaelewa kabisa mpaka baadae kabisa na mafundisho yao mpaka leo yanatumika. Sitaki kuamini kuwa na Prof.Lipumba kwa sababu ya U-Profesa wake ndiyo maana labda simuelewi!!!!!.
Ndiyo maana kwa sababu ya elimu yangu ya chini,huwa siwaelewi kabisa baadhi ya wasomi wanaonizidi kielimu. Kwa mfano, katika hili Prof.Lipumba simuelewi Dr.Bana naye huwa najitahidi sana kumsikiliza nimekuwa kila muda nashindwa kumwelewa akiwa anaongelea katika baadhi ya maswala ya kitaifa. Dr.yule aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa MOROGORO na kuondolewa na Rais Magufuli naye sikumwelewa kabisa mpaka saaizi sijawahi kabisa kumwelewa. Nakumbuka aliitisha vyombo vya habari na kusema anaomba asamehewe kwani alijutia makosa yake na kusema; Nimekosa Sana, Nimekosa Mimi, analinena kwa kusema asamehewe sana kwani ametoka familia masikini sana na hana pa kushika kabisa.. Huyo ni Dr.na hapo alitoka kuwa Mkuu wa Mkoa na nyuma aliwahi kushika nyazifa mbalimbali.
Ningekutana naye Prof,Lipumba ningemshauri aachane na Uenyekiti wa CUF kwani binafsi naona inapunguzia HESHIMA NA UTU aliokuwa naye kwa Jamii.
Mwisho tumwombe Mwenyezi Mungu atujalie HEKIMA NA BUSARA hata kama bado tuko katika hali ngumu zaidi katika kupambana kujitafutia riziki zetu. Cha msingi ni kumuomba Mwenyezi Mungu akupe HEKIMA NA BUSARA ZAIDI.
By S.N.Jilala/JF
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment