Kumbukumbu hiyo hufanyika kila mwaka tangu Mwalimu Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alipofariki tarehe 14 Oktoba 1999 alipokuwa kwenye matibabu nchini Uingereza.
Licha ya Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuarifu kwamba, Mama Maria Nyerere, mke wa mwalimu angehudhuria sherehe hizo, hakwenda.
Taarifa ya Mtaka aliyoitoa tarehe 5 Oktoba mwaka huu ilieleza kuwa, Mama Maria Nyerere pamoja na familia yake, wangefikia Nyamuata ambazo ni nyumba za Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadaye Mtaka alibadilisha makazi ya Mama Maria angefikia kwenye Hoteli ya Sumayi jambo ambalo lilithibitishwa na viongozi wasimamizi wa hoteli hiyo.
Pamoja na taarifa za Mtaka pia uthibitisho wa uongozi wa Sumayi kwamba, Mama Maria Nyerere angefikia kwenye hoteli hiyo kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, hawakufika.
Familia ya Mwalim Nyerere imekuwa ikishiriki maadhimisho hayo ambayo ni ya kitaifa kwenye maeneo mbalimbali tangu kufariki kwa Mwalimu Nyerere.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya Mwalimu Nyerere zinaeleza kutopata mwaliko wowote kutoka katika Serikali ya Rais John Magufuli ili kuhudhuria sherehe hizo.
Wakati serikali ikiendelea na maadhimisho yake mkoani Simiyu, familia ya Mwalumu Nyerere ilifanya ibada Maalumu katika Kanisa la Katoliki, Butiama.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Sospiter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na kwamba alimwakilisha Rais John Magufuli.
Wengine waliohudhuria ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini na Shyrose Bhanji Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA).
Chanzo: Mwanahalisi
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment