Oct 3, 2016

JOHN Mnyika Matatani...Nyumba Kupigwa Mnada Kwa Kushindwa Kulipa Deni

John Mnyika
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amedaiwa kuwaacha njia panda wadhamini  (majina tunayo) ambao walikubali kuidhamini kampuni ya Testa ambayo yeye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini.

Inadaiwa kwamba Mbunge huyo alichukua uamuzi wa kujiondoa kwenye kampuni hiyo baada ya kuona  inashindwa  kulipa deni la Sh milioni 300 ambalo linatokana na riba ya mkopo wa Sh milioni 222 ambazo   Testa ilikopeshwa na benki ya Standadr Chartered.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA limezipata zinaeleza kuwa kwa miaka mitatu sasa wadhamini hao wamekuwa wakihangaika kutafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye deni hilo.

Inaelezwa kuwa nyumba za wadhamini hao ambazo ziliwekwa rehani   kupata mkopo huo zipo kwenye hatihati ya kupigwa mnada  kufidia deni hilo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, kampuni ya Testa ilikuwa ikijihusisha na uwakala mkubwa wa masuala ya huduma za fedha kupitia simu za mkononi.

Chanzo chetu hicho kilieleza kwamba Mnyika ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo na ambaye aliridhia kukopwa  kiasi hicho cha fedha katika benki hiyo.

“Mnyika alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, alikuwa na hisa nyingi kuliko wenzake – ya zaidi ya asilimia 50 – na kwa nafasi hiyo ya uenyekiti saini yake ndiyo ilikuwa inatambulika kule benki ili kuchukua mkopo,” kilieleza chanzo hicho.

Kilieleza pamoja na Mnyika kudaiwa kujiondoa  katika kampuni hiyo siku nyingi hata hivyo hakuwasiliana na wadhamini wake na hata benki hiyo kuwaeleza juu ya uamuzi wake huo.

Nyaraka muhimu ambazo MTANZANIA imeziona zinaonyesha kampuni hiyo ilikubaliwa kukopeshwa fedha hizo baada ya kikao cha bodi   Januari 25, 2012,   Mnyika akiwa mwenyekiti.

“Kikao cha bodi ndicho kilichokuwa na uamuzi juu ya shughuli za kampuni ikiwamo masuala ya kukopa. Januari 25, 2012 wajumbe walikaa na kukubaliana kukopa. Mnyika akiwa mwenyekiti aliidhinisha kwa kutia saini yake Mei 11, 2012 ndipo kampuni ikakopeshwa,” kilieleza.

Nyaraka nyingine kutoka benki hiyo ambazo MTANZANIA imeziona zinaonyesha awali  kampuni hiyo  ilikuwa ikirejesha vizuri deni hilo,  tangu Agosti 31, 2012 hadi   Februari 28, 2014.

Nyaraka hizo zinaoneysha kuanzia Machi 31, 2014  kampuni ilishindwa kurejesha fedha zozote hadi kufikia  Julai 31, mwaka huu ambao ndiyo ulikuwa mwisho wa kurejesha mkopo huo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, wadhamini hao walikuwa wakifuatilia maendeleo ya kampuni hiyo kwa mmoja ya wakurugenzi (jina tunalo) na walikuwa wakijibiwa kuwa kampuni inaendelea vizuri.

“Miezi sita baada ya kuzungumza na Mkurugenzi huyo, benki ilituma wawakilishi wake kwa wadhamini na wakakabidhiwa barua ya kuwajulisha kuwa deni halijalipwa na nyumba zao zitapigwa mnada kulifidia,” kilieleza.

Chanzo hicho kilieleza kuwa kutokana na hali hiyo, mmoja wa wadhamini hao amekwisha kufanya juhudi za kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, chama ambacho anatokea Mbunge huyo  kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

“Alishawahi kumfuata Dk. Willbrod Slaa (alipokuwa Katibu Mkuu wa Chadema), Freeman Mbowe (mwenyekiti) na hivi karibuni ameenda kuomba kuonana na Edward Lowassa (Mjumbe wa Kamati Kuu) na iwapo hatafanikiwa yeye na mwenzake wamepanga kuchukua hatua nyingine ambazo hawajaziweka wazi,” alisema.

MTANZANIA ilipomtafuta Mnyika kwa   simu kuzungumzia suala hilo    simu yake  iliita bila kupokewa na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi alijibu baadhi ya maswali kama ifuatavyo;

MTANZANIA: Habari mheshimiwa, naitwa… kuna taarifa kuwa nyumba za wadhamini wako zinapigwa mnada kwa sababu umeshindwa kurejesha mkopo wa zaidi ya Sh milioni 200, nini kauli yako juu ya tuhuma hizi?

Mnyika: Hakuna mtu yeyote aliyeweka nyumba kunidhamini waulize wakuambie ukweli.

MTANZANIA: Kuna nyaraka ambazo tunazo moja ikiwamo ya makubaliano ya bodi ya wakurugenzi ambayo wewe ulisaini ukiwa mwenyekiti na ilionyesha wadhamini sita zikiwamo nyumba mbili zilizopo Bunju na Mmbweni.

Mnyika: Iliyokopa ni kampuni si mimi na niliondoka kwenye hiyo kampuni tangu mwaka 2013 bila kupokea fedha yoyote binafsi… hivyo ni vizuri ukawatafuta wenye hiyo kampuni kuwauliza na waulize pia hao wadhamini walinufaika vipi na hiyo mikopo na nani aliwafuata waweke hati zao.

MTANZANIA: Mheshimiwa wewe ulikuwa nani kwenye hiyo kampuni, wajibu wako ulikuwa upi na uliondoka vipi na nani ni wamiliki wa hiyo kampuni?

Mnyika hakulijibu swali hili na alipoombwa kupigiwa hakujibu.  Vilevile,  alipopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa hadi gazeti hili linakwenda mtamboni jana usiku.

Source: Mtanzania

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger