Oct 25, 2016

RUSHWA Yawaponza Vigogo wa Bandari Dar

Aliyekuwa mkuu wa mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe, amefikishwa tena mahakamani akikabiliwa na kesi mpya ya kuomba rushwa ya dola za Marekani milioni nne.

Mgawe na wenzake watatu ambao walikuwa mahabusu tangu Ijumaa, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu hii na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili Mkuu wa serikali, Mutalemwa Kishenyi, aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa uhandisi TPA, Bakari Kilo, Meneja wa manunuzi TPA, Theophil Kimaro (54) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya DB Shapriya Ltd, Kishor Shapriya.

Kishenyi alidai mshtakiwa wa kwanza hadi wa tatu wanadaiwa kati ya mwaka 2009 na 2012 mahali pasipojulikana, wakiwa katika nyadhifa zao, kupitia wakala wa Kampuni ya DB Shapriya Ltd waliomba rushwa ya dola za Marekani milioni nne.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuomba kiasi hicho cha fedha kama kishawishi cha kuiwezesha kampuni hiyo kupata zabuni ya kuweka boya la kushushia mizigo (SPM) na bomba la mafuta RAS TPA, Mji Mwema.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa wa nne, Shapriya, anadaiwa kati ya mwaka 2009 na 2012 alitoa rushwa kwa Mgawe, Kilo na Kimaro, ikiwa ni kishawishi cha kupata zabuni hiyo. Washtakiwa walipotakiwa kujibu mashtaka hayo, wote walikana na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Upande wa Jamhuri ulidai hauna pingamizi kwa washtakiwa kupata dhamana, isipokuwa watimize masharti watakayopewa na mahakama.

Hakimu Simba alikubali kuwapa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili, watakaosaini dhamana ya maandishi ya shilingi milioni 500 na washtakiwa wanatakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani.

Walitimiza masharti ya dhamana na kesi iliahirishwa hadi Novemba 7, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mgawe anakabiliwa na kesi nyingine katika mahakama hiyo ambayo iko katika hatua ya kutolewa hukumu.

Katika kesi hiyo, Mgawe na wenzake wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa zabuni ya upanuzi wa gati namba 13 na 14, katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd (CCCC), bila ya kutangaza zabuni.

Januari 2013, aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliwaondoa katika nyadhifa zao Mgawe na wenzake baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu na kuisababishia Serikali hasara kubwa.

Mbali na Mgawe, wengine waliotimuliwa kipindi hicho ni aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu, Julius Mfuko, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ngamilo na Meneja Kituo cha Kupakulia Mafuta, Tumaini Massaro.

Dk. Mwakyembe alidai Mgawe alizembea na kuruhusu kuwapo kwa muda mrefu utaratibu usiofaa wa upokeaji na uondoshwaji bandarini wa mafuta machafu.

Katika tuhuma hiyo, Mgawe anadaiwa kuachia kiasi kikubwa cha mafuta safi kuibwa na kushindwa kudhibiti kiwango cha utoaji wa mafuta machafu bandarini kinyume na mikataba iliyopo.

Tuhuma ya pili iliyomwondoa Mgawe ni ufanisi duni ambao Dk. Mwakyembe alifafanua kuwa alishindwa kudhibiti wizi wa mizigo na mali ya mamlaka uliokithiri bandarini.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, pia alikiuka sheria na utaratibu. Anadaiwa kuingia mkataba na CCCC bila kuishirikisha Bodi ya Zabuni ya Mamlaka.

Pia anadaiwa kuongeza mishahara kwa asilimia 15 bila idhini ya Waziri wa Uchukuzi, hivyo kukiuka utaratibu uliowekwa na sheria.

Tuhuma zilizomng’oa Koshuma kwa mujibu wa Dk Mwakyembe ni nne, ikiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka.

Anadaiwa pia kuruhusu michakato ya zabuni bila kufuata utaratibu kwa kisingizio cha miradi mikubwa, kuwa na ufanisi duni, ambapo akiwa Mjumbe wa Bodi ya Zabuni, alishindwa kuijulisha Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi ya Umma (PPRA), kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Ununuzi.

Ukiukwaji huo ulifafanuliwa kuwa ni wa kuruhusu Mamlaka kuingia mkataba wa kibiashara na CCCC bila kushirikisha Bodi ya Zabuni na kushindwa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka katika udhibiti na uendeshaji.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger