Bodi ya Shirika la Changamoto za Millenia (MCC), imefunga rasmi shughuli zake jijini Dar es Salaam Septemba 29, ikiwa ni miezi sita tangu lilipositisha msaada wa fedha kwa Tanzania.
Chanzo cha habari kimelieleza Mwananchi kuwa, bodi hiyo ilifunga huduma zake nchini Alhamisi iliyopita, hali inayoashiria kuwa ni mwisho wa majadiliano kati yake na Serikali kuhusu ufadhili huo.
Machi mwaka huu, MCC ilitangaza kusitisha ufadhili wa Dola 472.8 Marekani (Sh1 trilioni) kwa Serikali ya Tanzania.
Shirika hilo lilifikia uamuzi huo kwa kile walichodai kutoridhishwa na marudio ya uchaguzi wa Zanzibar na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.
Bodi hiyo ilisema Tanzania imeshindwa kutimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili, hivyo haitapokea msaada wa awamu ya pili wa kiwango hicho cha fedha.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment