Oct 25, 2016

Tanzania Yapata Mkopo Wenye Masharti Nafuu Wa Zaidi Ya Shilingi Bilioni 300 Kutoka Benki Ya Maendeleo Ya Afrika (Afdb) Na Serikali Ya Korea

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akitia saini makubaliano ya uteuzi wa mradi utakao fadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Korea, wenye thamani ya dola Milioni 50 za Marekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18 zitakazotumika kujenga njia ya usafirishaji umeme kwanjia ya gridi ya Taifa, yenye msongo wa kV 400 katika ukanda wa kaskazini Magharibi itakayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Mkoani Kigoma.

TANZANIA, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Korea ya Kusini zimetiliana saini makubaliano ya pamoja kutekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya umeme gridi ya Kaskazini Magharibi inayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Kigoma, yenye msongo wa kV 400 mbapo Serikali ya Korea imeahidi kutoa Dola za Marekani milioni 50 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18, kwa ajili ya kugharamia mradi huo.

Hali kadhalika, Tanzania na Benki ya Exim ya Korea, zimesaini  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam.

Kwa upande wa Tanzania, Makubaliano pamoja na Mkataba vimesainiwa na Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) Waziri wa Fedha na Mipango kwa niaba ya Serikali, Oktoba 25, 2016 Jijini Seoul nchini Korea Kusini huku upande wa AfDB, aliye saini ni Rais wa Benki hiyo Adesina Akinwumi, na kwa upande wa Benki ya Exim, mkataba huo umesainiwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki hiyo Lee Duk-Hoon.

Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano na mkataba huo, Dkt. Mpango amesema makubaliano na mkataba vilivyosainiwa vina manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.
Pause ( Kwa TV) Waziri Mpango-akizungumza kuhusu umeme
“Wananchi wa Upande ule waanze kufurahia kwamba maendeleo yanakuja na hasa tunaposema maendeleo ya viwanda ambavyo ni lazima vitumie umeme, na kwamba mradi huu unatarajia kupelekwa hadi Mbeya” Amesisitiza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango, amesema kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa pia kwa kuwa serikali imedhamiria kuufungua ukanda wa Magharibi mwa Tanzania, kwa upande wa viwanda vya aina mbalimbali.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uwekezaji) wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania-TANESCO, Decklan Mhaiki, amesema mradi wa umeme wa Nyakanazi hadi Kigoma utakuwa na urefu wa kilometa 280 na utakapo kamilika utaondoa changamoto ya shirika hilo kuzalisha umeme unatumika katika ukanda huo wa Magharibi hususan Kigoma, kwa kutumia majenereta ambayo uendeshaji wake ni ghali na umeme wake si wa uhakika.

“Kuleta laini kama hii, kwanza itapunguza gharama kubwa, na umeme wa ziada utakao zalishwa tunaweza kuuza nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, upande wa pili wa Ziwa Tanganyika, lakini kikubwa ni kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika” ameongeza Bw. Mhaiki.

Akizungumzia mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya maji taka Jijini Dar es salaam, Dkt. Philip Mpango, amebainisha kuwa mradi huo unatarajia kuwa na tija kwakuwa utatatua changamoto ya majitaka kutuama mitaani hasa wakati wa mvua na kusababisha magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu.

Akifafanua kuhusu mradi huo, Mchumi ambaye pia ni  Afisa anayeshughulika na utafutaji wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Melckzedek Mbise, amesema kuwa mradi wa maji wa Ruvu  unatarajia kuongeza wingi wa maji Jijini Dar es salaam, utakaosababisha uzalishaji wa maji taka pia kuongezeka, hivyo mradi huo wa kuondoa maji taka umekuja  wakati muafaka.

“Mradi huu umekuja wakati muhimu na mkopo una masharti nafuu sana” Amesisitiza Bw. Mbise.
Naye Afisa Mkuu wa utafutaji rasilimali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Sabra Issa Machano, amesema kuwa  kati ya nchi 54 za Kiafrika zinazohudhuria mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na Afrika, Mjini Seoul Korea, ni nchi nne tu zilizopewa mkopo na ufadhili ambazo ni Kenya, Uganda na Ethiopia, huku Tanzania ikipewa kiasi kikubwa zaidi cha fedha jambo linaloonesha kuwa Tanzania inakubalika Kimataifa.



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee Duk-Hoon, wakipeana mikono baada ya kusaini  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika, unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger