Kiba alitumbuiza nyimbo mbili tu kabla ya mic aliyokuwa anaitumia kuonekana kupata mushkeli/kuzimwa na kumlazimu kuondoka jukwaani na muda mchache baadae akapanda Chris Brown.
Akiongea katika kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya Kenya na Willy Tuva, Sallam amekanusha moja kwa moja kuhusika kwenye tukio hilo.
“Pale mimi nilienda kuangalia show na kuja kufanya connection zangu ambazo zinaendelea, tulikuwa na WizKid Tanzania alivyotoka kufanya show ya Fiesta tulikuwa naye Dar es salaam na akakutana na Diamond. Pia meneja ambaye anasimamia kazi za Diamond West Africa ni Mr Sande ambaye ndiye meneja wa WizKid,
kwa hiyo shughuli zote nyingine ambazo zinafanyika West Africa yeye ndiye anashughulikia hivyo vyote. Kwa hiyo hiyo ndio kazi ambayo imenileta, na uwepo wangu wote nilikuwa na team ya WizKid,” alisema Sallam.
Aliongeza, “Kwa hiyo mimi kuja hapa kilikuwa ni kitu cha kawaida kabisa, kwa sababu kulikuwa na mameneja wa wasanii wengine ambao wasanii hao hawakuwa kwenye show, sijui kama Sauti Sol waliperform lakini najua hawakuperform lakini walikuwepo pale pamoja na mameneja wao, wasanii wengi walikuwa na mameneja wao pale.
Unaweza kuona ni jinsi gani kulikuwa na opportunity ya kuja pale na kukutana wadau mbalimbali pamoja na kujifunza vitu wanavyofanya wenzetu. Sasa kama unanituhumu mimi kuwepo pale, usinichukie mimi kwa sababu mimi nakuwa na access, kama kuna kitu unahitaji kwangu nifuate usiogope, kwa sababu sisi wote ni watanzania.
Pia wakati anaperform mimi sikuwepo kabisa pale, na hicho kitu media zote ziliona kwa sababu kamera nyingi zilikuwa kwangu, na wakati anafanya show AliKiba mimi niliwa mbali kabisa,”
Akielezea kilichotokea mkapa AliKiba akazimiwa Mic, Sallam alisema “Alifanya show Vanessa Mdee baada ya Vanessa Mdee alitakiwa Ali apande, kwa dakika 30 show ilisimama wakimngoja AliKiba, AliKiba hataki kufanya show mpaka WizKid afanye show halafu yeye ndo afanye,
sawa mimi sijui hizo habari ambazo zinasikika AliKiba ni mkubwa kuliko WizKid, baada ya dakika kadhaa nikamuona Sande anasema acha tuwape dakika 10 kama asipopanda sisi tutampandisha msanii wetu, baada ya hapo Mr Sande akamwambia stage meneja lets go with WizKid, Sande akamchukua msanii wake na kumpandisha kwenye stage.
Ndipo na mimi nikapanda kwenye stage kwa sababu nilikuwa na access nilikuwa nao, baada ya kumaliza WizKid tulishuka wote, niliiona team ya AliKiba wakati wanaswali pale chini, kwa hiyo wale walikuwa wanapanda sisi tunashuka, kwa hiyo mimi niliondoka kabisa kwenye stage.
WizKid alipanda kwenye gari na Dj Mafolisa, mimi na Sande tuliingia kwenye room, na muda huo sisi tulikuwa mita 50 kutoka kwenye stage hatuelewi nini kinatokea. Kitu ambacho mimi nilisikia kule kulikuwa na ugomvi mwingine, security wa Chris Brown na stage meneja wanagombana kutaka AliKiba ashuke, kwa sababu ratiba yao Chris Brown anatakiwa show yake iishe saa saba.
Chris alishasema anataka kuperform saa 5 kamili awe kwenye stage, kwa hiyo tayari walikuwa wameshachelewa, kwa hiyo kitu kingine ambacho nilisikia muziki umezimwa, Chris anaenda kufanya show, akapigiwwa simu Sande na WizKid njoeni hapa, tukaenda,” Tazama Video Nzima Hapa:
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment