Wataalamu hao wanatarajia kuangazia mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo, kujadili mikakati ya afya ya uzazi, afya za watoto wachanga na vijana.
Pia, watajikita kujadili magonjwa sugu yasiyoambukiza, ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele, usalama wa maji na usafi wa mazingira.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela alisema mada 220 zitawasilishwa na kujadiliwa katika kongamano hilo la siku tatu, huku mada kuu ikiwa ni ‘Uwekezaji katika utafiti wenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia’.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment