Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Lazaro Mambosasa |
Akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Iringa Mvumi kilichopo tarafa ya Makang'wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma eneo ambalo mauaji hayo yalifanyika, kamanda wa polisi mkoani Dodoma Lazaro Mambosasa amesema kuwa wanaoshikiliwa ni wanawake tisa pamoja na wanaume 21 ambao walihusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji nayo.
Kamanda amesema kuwa watu hao wanashikiliwa kwa mahoajiano kwani ndiyo waliokuwepo katika eneo la tukio wakati maafisa hao wanauawa.
Aliwataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni dereva wa gari walilokuwa wakisafiria Nicas Magazini pamoja na watafiti wawili ambao ni Teddy Nguma na Faraji Mafuru.
Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kufuatia mauaji nayo ili waweze kupisha uchunguzi wa tukio hilo.
Aliwataja waliosimamishwa kazi kuwa ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Godfrey Mnyamala pamoja na afisa utumishi wa halmashauri hiyo Salum Makila kwa kosa la kupokea utambulisho wa watafiti hao lakini hawakusambaza taarifa za ujio wa watafiti hao kwenda kwa viongozi wengine ngazi za chini.
Maafisa hao walikutwa na umauti wakati wanatekeleza majukumu yao ya kila siku baada ya baadhi ya wananchi kuwahisi kuwa ni wanyonya damu waliovamia kijiji hicho ambapo waliwavamia na kuwapiga kwa kuwakatakata na mapanga na kisha kuichoma miili yao pamoja na gari waliyokuwa wakiisafiria.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment