Kijana huyo ambaye anadaiwa kutumia jina la ‘Shilolekiuno_official’ kwenye mtandao huo amekuwa akiwatukana baadhi ya mastaa akiwemo Diamond Platnumz pamoja na familia yake, mabosi wa WCB na Wema Sepetu, amefikishwa kwenye kituo cha polisi cha Oysterbay.
Kupitia mtandao wa Instagram, Sallam ambaye ni meneja wa Diamond ameandika,
“Kwa watu wote kama ulitukanwa na huyu ambae anaejiita @shilolekiuno_official kwa sasa yupo chini ya mikono ya sheria, Kama una mashitaka yoyote fika Oyster Bay Polisi, Vizuri ametaja watu wanaemtuma afanye hivyo! Na kuwasaidia wale ambao wanajiamini kuwa hawawezi kujulikana basi kwa taarifa yenu Serikali ina mkono mrefu sana! Eti Jana alikuwa anamuita Diamond “Simba” 😂😂😂.”Hata hivyo kamanda wa polisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, “Hatujamkamata na hatuna mtu kama huyo kituoni kwetu. Tuna vijana wengi ambao wamekamatwa wanamakosa kama hayo, jina kama hilo uliloniuliza halipo hapa kituoni kwetu labda kwenye kituo kingine.”
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment