Nov 29, 2016

Mzee wa Upako Awageukia Waandishi wa Habari

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, amesema licha ya kupatwa na mikasa mbalimbali, hajavunjwa moyo bado anaendelea na kwamba huu ni mwaka wa kucheka sawa sawa na lilivyo jina lake.

Alisema hayo ikiwa ni baada ya kuingia matatani na vyombo vya dola kutokana na kudaiwa kumfanyia vurugu jirani yake katika tukio lililotokea mwishoni mwa wiki na kuripotiwa na mitandao ya kijamii, huku picha zikimuonesha akirushiana maneno makali na jirani huyo aliyesikika sauti.

Alisema haiogopi jela, bali anaogopa kuvunja sheria za nchi na wala alipokamatwa na Polisi haikumtisha wala kumvunja moyo, kwani viongozi wa dini wamekula kiapo hadi kufa. Mchungaji huyo aliyasema hayo Jumapili hii wakati akihubiri katika kanisa hilo lililoko Ubungo jijini Dar es Salaam, ambako alitumia takribani saa moja na kutoa mahubiri huku akisema hayumbishwi na matukio anafanya kazi ya injili.

Mara baada ya kuingia ibadani hapo, Mchungaji Lusekelo alianza kwa kipindi cha kusifu huku waumini waliofurika katika kanisa hilo wakimiminika kwenda mbele kutoa sadaka kisha kuanza mahubiri.

Aliwaambia asingependa kusema chochote kuhusu sakata lililomkuta, bali wakimaliza kusema yeye ndipo atakapoanza kusema na kwamba mwaka huu hawezi kuumaliza kwa huzuni, bali ni wa furaha kama jina lake lijulikanavyo kwa kabila la Kinyakyusa na wakati wote ana furaha.

“Sitaki kuzungumzia huko sana, ninafanya kazi ya Mungu, watu wanataka kuuza magazeti wanaandika taarifa zangu (Lusekelo), huku wakiandika vichwa vya habari eti Askofu matatani… matatani babu yao,” alisema Mzee wa Upako huku akisisitiza kuwa, “mbona yapo matukio makubwa zaidi katika kanisa lake na hayapewi kipaumbele kwa habari za mbele kama ilivyokuwa kwa tukio lililomkumba.”

Alihoji kuwa vyombo hivyo vya habari vimekosa taarifa mbalimbali za uchumi hata za biashara zilizopo nchini na kuamua kuandika kwa wingi na kwa uzito, akidai kwa kufanya hivyo kumeendelea kumpa umaarufu mzito.

Aidha, alisema wapo waliosema kuwa Mzee wa Upako alikuwa anatukana, alidai kuwa matusi yake yote ni maandiko na anayetaka ufafanuzi wowote akipata nafasi amuulize yameandikwa katika vitabu gani li apate kuelewa.

Alisema mpumbavu sio tusi hayo ni maelezo na Yesu alitukanwa sana, na hata ushenzi si tusi lina maana pana ya kwamba huna hofu ya Mungu, mjinga ana dhambi ya mauti, inayomsubiri kwenda peponi.

Hata hivyo, aliwausia waumini wa kanisa hilo kuwa kamwe wasimtukane mtu kwa umbo ama rangi yake kwa kuwa hakupenda kuzaliwa hivyo na waishi hivyo kwa kutenda mema kwa kuwa ufalme wa Mungu watauona.

Alisema tangu kutokea kwa tukio amekuwa akipigiwa simu na watu ambao hakuwategemea huku waandishi wakimtaka kuzungumzia chochote wakiwamo waandishi wa habari ambao alisema walikuwamo ndani ya kanisa hilo jana.

Akifafanua kilichotokea siku hiyo, alieleza kuwa alitoka saa 11 alifajiri bila kufafanua alikuwa akitokea wapi, ndipo alipokutana na watu wawili akiwemo Mmasai na dada mmoja alipowauliza wanatokea wapi katika eneo hilo ambalo wakazi wengi wa huko hutoka na magari yao, ndipo ugomvi ulipoanzia.

“Hawa watu wa magazeti wanataka kuuza magazeti, barabara hiyo nimeijenga mimi hivyo nilikuwa na haki ya kuwauliza maana ni kibarabara… washenzi wakubwa wanaandika tu, halafu wanasema nimewatukana majirani kule hakuna jirani hajui wanaingia saa ngapi na wanatoka saa ngapi na hakuna hata habari za asubuhi. Kila mmoja anatumia gari lake,” alieleza Mzee wa Upako.

“Hata vijana wa Sirro waliponikamata haijaniumiza, kunitisha wala kunivunja moyo kwani hata Yesu alikamatwa. Viongozi wa dini wamekula viapo hadi kifo, hawaogopi jela, anaogopa kuvunja sheria za nchi,” alisema.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger