Nov 15, 2016

Wanachama 17 Chadema Waliokuwa Wakipanga Maandamano ya UKUTA Wafutiwa Kesi Mahakamani

Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imewaachia huru viongozi na wanachama 17 wa Chadema walikokuwa wakikabiliwa na mashitaka ya kujaribu kushawishi kutenda kosa Agosti 25 katika ofisi ya wilaya ya chama hicho Mnadani mjini hapa.

Wanachama waliachwa jana na Hakimu Tumaini Marwa aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo baada ya upande wa mashitaka chini ya Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Nassib Swedy kushindwa kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo huku wakitoa sababu mbalimbali.

Swedy alidai kuwa  washitakiwa hao wakiwa kwenye ofisi yao siku hiyo saa 7 mchana walipanga kufanya maandamano na mikutano ya Ukuta, ambayo ingehatarisha amani na utulivu wilayani humo na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, washitakiwa hao ambao awali walifikishwa mahakamani hapo Agosti 26 chini ya ulinzi mkali wa Polisi, walikana mashitaka na kunyimwa dhamana, walidhaminiwa Septemba 2 baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika ambaye alisaini bondi ya Sh milioni tano.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Marwa alitupilia mbali maombi ya upande wa mashitaka yaliyokuwa yakiomba ahirisho la kesi hiyo kwa mara nyingine ukidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Alisema amri ya mwisho aliyoitoa ilikuwa ahirisho la Novemba 4 hivyo upande wa mashitaka umeshindwa kutekeleza amri ya Mahakama na kwa maana hiyo, anawaacha huru washitakiwa wote chini ya kifungu cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kifungu cha 225 (5) sura ya 20.

“Kifungu hiki kilichowaacha huru washitakiwa hakizuii Polisi kuwafikisha mahakamani tena washitakiwa kwa kosa hilo, iwapo watakuwa wamekamilisha uchunguzi juu ya shauri linalowakabili,” alisema Hakimu Marwa.

Hata hivyo, wakati uamuzi unatolewa wakili wa washitakiwa hao, Martine Sabini aliyekuwa akiwakilisha washitakiwa wote hakuwapo mahakamani, lakini alikuwa ameshawasilisha ombi mbele ya Mahakama hiyo kuomba waachiwe huru kwa sababu ya upande wa mashitaka kushindwa kukamilisha upepelezi kwa muda mwafaka.

Walioachiwa huru ni pamoja na  Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Maswa, Peter Shiyo (39), Katibu wa Chadema wa Wilaya, Flora Msuka (31), Katibu wa Bawacha wa Wilaya, Elias Matondo (37) na  Katibu Mwenezi wa Maswa Mashariki, Waziri Peter (46).

Wengine ni  Bundala Baya (30), Edward Makoye (63), Sylvester Ngwege (60), Frank Makaranga (31), Selemani Kombe (39) na Mapambano Jackson (37).

Pia Nkuba  Magwila (40), Ndebile Paul (27), Edgar Ngasa (32), Lucas Nkuba (39), Laurent Mahembo (36) na Mwajuma Said (40).

Baada ya kuachwa, Shiyo aliishukuru Mahakama kwa kutenda haki akilitaka Jeshi la Polisi kuacha kunyanyasa viongozi wa vyama vya upinzani kwa kufanya kazi kwa hisia na matokeo yake, wanaitia aibu Serikali kwa kushindwa kesi mahakamani.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger