Matindi alisema hatua hiyo ya kununua ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine abiria 242, italifanya shirika hilo kuendelea kuimarika, kutambulika na kuheshimika tofauti na hali ilivyokuwa miezi mitatu iliyopita.
“Ndege hizo aina ya jet zitawasili Juni, zina uwezo uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi na kwenda masafa ya mbali tofauti na Bombadier Q400 ambazo Watanzania walikuwa wanazikejeli,” alisema mkurugenzi huyo.
Wakati kampuni binafsi za ndege zikilamikia kudorora kwa biashara kutokana na gharama za uendeshaji, Matindi alisema kilio hicho kinawahusu wote. “Sisi tunalalamika kimyakimya na kuzifanyia kazi changamoto, hata ATCL inalipa kodi, mafuta pekee hugharimu asilimia 25 hadi 30 ya gharama za uendeshaji,” alisema Matindi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment