Ikiwa Manchester City watashinda mchezo wao dhidi ya Swansea City basi haijalishi Man United watapata matokeo ya namna gani dhidi ya Bournemouth – United wataikosa michuano ya ulaya mara ya pili ndani ya misimu mitatu mfululizo.
Hii ni habari mbaya kwa mashabiki wa United lakini ni habari mbaya zaidi kwa mabosi wa MANCHESTER UNITED kwa sababu watapoteza kiasi cha angalau £30m (zaidi ya billioni 90 za madafu) kwa kuikosa michuano hiyo tajiri barani ulaya.
CEO wa klabu hiyo Ed Woodward amewathibitishia wanahisa wa klabu hiyo kwejye mkutano wa leo jioni lakini pia akawapa uhakika wa kupata faida.
Lakini pia ikitokea United wakaikosa michuano hiyo msimu wa pili mfululizo, wadhamini wa jezi zao Adidas watapunguza asilimia 30 ya £750m za dili lao na klabu hiyo.
Kikosi cha Louis van Gaal kilikuwa na nafasi ya kuipiku Man City jumanne iliyopita lakini wakashindwa kupata ushindi katika mchezo muhimu wa ligi dhidi ya West Ham United.
Ripoti zinasema endapo tu United watashindwa kufuzu kucheza Champions League msimu ujao basi kibarua cha Van Gaal huenda kikaota nyasi na Jose Mourinho akatangazwa kumrithi pale Old Trafford.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:



0 [disqus]:
Post a Comment