Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa ameviagiza vyombo vya Uchunguzi ikiwemo taasisi ya kupambana na Kuzuia rushwa Takukuru kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kufuatia gharama kubwa za ujenzi ambapo mpaka sasa Ujenzi wake umefikia Shilingi Billion 12 huku wahusika wakionekana kukopa katika benk mbili kwa viwango tofauti kwa ajili ya ujenzi huo.
Mhandisi wa Manispaa ya Temeke Injinia Benjamini Maziku alijikuta katika wakati Mgumu baada ya kuulizwa maswali na Mkuu wa mkoa kuhusu Mkandarasi wa jengo, michoro na kushindwa kutoa taarifa kamili kuhusu ujenzi huo ikiwemo amri ya Kusimamisha ujenzi tangu januari…lakini amri hiyo ikapuuzwa na jengo kuendelea kujengwa na kushindwa kuchukua hatua.
Akizungumza na Waandshi wa habari Bw,Makonda amesema katika mchoro wa awali majengo hayo yalionekana kuwa Mawili lakini yakaunganishwa kinyemela, pia yalikuwa ya ghorofa kumi kila moja lakini yamejengwa Ghorofa nane huku fedha zilizoombwa katika mabenki zikiwa zimetofautiana na kuzidi kiasi cha ujenzi wa jengo hilo hali inayotia mashaka ya kufanyika kwa Ubadhilifu wa Fedha za Umma.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment