May 3, 2016

Rais Magufuli Adaiwa Kuwa ni Mkandamizaji

SERIKALI ya Rais John Magufuli inalalamikiwa kutokana na serikali yake kujenga tabia ya ukandamizaji kwa wanahabari,anaandika Moses Mseti.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kusikitika kutokana na kujengekwa kwa tabia hiyo na kwamba, kitendo cha kunyang’anya uhuru na haki ya wananchi kupata habari hakikubaliki.
Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amesema, kutokana na ukandamizaji unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli hauvumiliki.

Moja ya mambo na sheria zinazoonekana kuvikwaza vyombo vya habari nchini ni waandishi wa habari kuzuiwa kuchukua habari moja kwa moja ‘live’ wakati wa vikao vya bunge la bajeti na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 pia kutungwa kwa sheria zinazokandamiza vyombo vya habari na waandishi wake.

Akizungumza leo wakati wa kilele cha Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) amesema,  kitendo cha serikali kuwazuia waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonesha ‘live’ bunge hilo ni sawa na uvunjwanji wa Sheria na Haki ya Kupata Habari huku akidai kitendo hicho hawakubaliani nacho.
“Mwaka 1992 sheria za habari zilikuwa 17 lakini sasa hivi zimetengenezwa tengenezwa tu hadi kufikia 26 hiyo yote ni ya Serikali kutaka  kuvibana vyombo vya habari visifanye kazi zao kwa uhuru, kitendo ambacho ni kibaya sana kwa ukuaji wa tasnia hii,” amesema Balile.

Pia Balile ametolea mfano sheria ya takwimu (The statistics act, 2013) ambayo anasema kuwa, sheria hiyo ipo kwa lengo la kumkandamiza mwanahabari na vyombo vya habari.
Na kwamba, kwenye kutekeleza wajibu wao na hawatarudi nyuma katika kutetea suala hilo mpaka pale litakapopatiwa ufumbuzi.

“Mfano kuna hili suala la takwimu ambalo linawanyima waandishi wa habari, kwamba kama mwandishi akiandika takwimu ambazo zitakuwa zimekosewa na mtoa taarifa, yeye ndie anaekuwa mhanga tatizo na wakati yeye kaandika,”alisema Balile.

Katika hatua nyingine Ubalozi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania umeeleza mambo 17 yanayolenga kulisaidia Taifa kupiga hatua ya maendeleo pamoja na vyombo vya habari nchini kukuwa kitaaluma kwa miaka 10.

Akiwasilisha malengo hayo 17 kwa wahariri, waandishi wa habari na wadau wa habari, Usiah Nkoma, Ofisa Habari UN amesema, malengo hayo yanakusudia kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi.

Nkoma ameyataja mambo hayo kuwa ni kutokomeza umaskini, kukomesha njaa, afya njema na ustawi, elimu bora, usawa wa jinsia, maji salama na safi, nishati mbadala kwa gharama ndogo, kazi zenye staha na ukuzaji uchumi.

Pia ametaja mambo mengine kuwa ni kukuzaviwanda na miundombinu, kupunguza tofauti za kiubinadamu, kuwa na miji na jamii endelevu, matumizi na uzalishaji wenye uwajibikaji, kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, kuendeleza uhai katika maji.
Nkoma ametaja mambo mengine kuwa ni pamoja na kulinda uhai wa ardhi, amani, haki na taasisi madhubuti na ushirikiano katika kufanikisha malengo hayo endelevu kwa ukuaji wa uchumi wa taifa na vyombo vya habari kwa ujumla.

“Malengo yetu nikuona kila mmoja akiwajibika kwa nafasi yake na waandishi wa habari kwenye taifa lolote lile wao ndio nguzo kubwa kwa ukuaji wa maendeleo yaTaifa hilo ni lazima kuwepo na mazingira salama,”alisema Nkoma.



Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger