Mrema ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuanzia mwaka 1990 hadi 1994 ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na EATV kuhusu hatua ya Rais Magufuli ya kutengua uteuzi wa waziri wa mambo ya ndani ya nchi kwa kosa la ulevi wakati akijibu maswali ya wabunge.
Mrema amesema kwamba nyazifa wanazopata mawaziri hawapaswi kubweteka kwa kuwa Rais amewaamini ili wamsaidie kutimiza majukumu na sii vinginevyo.
''Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ni moyo wa nchi, ni sehemu nyeti sana ikitetereka na usalama wa taifa unakuwa shakani sasa ukikutana na waziri amelewa asubuhi saa tatu muda wa maswali na majibu kutoka kwa serikali maana yake ni kukiuka sheria na vilevile kutomuheshimu Rais ambaye amekupa cheo hicho''-Amesema Mrema.
Aidha Mrema ameweka wazi kwamba watumishi wengi wa serikali wamejisahau kuanzia ngazi ya chini ambapo jambo hilo linazorotesha maeneleo ya taifa.
Pia ametoa wito kwa viongozi ambao wamepata dhamana ya kuongoza serikali kuhakikisha wanamsaidia Rais Dkt. John Magufuli ili nia yake njema ya kukomboa wanyonge ifanikiwe.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment