Jun 15, 2016

Mrema Amkingia Kifua Magufuli....Awataka Wapinzani Wamwache Achape Kazi

MWANASIASA mkongwe nchini na Naibu Waziri Mkuu mstaafu, Agustine Mrema amewataka wapinzani kumwacha Rais Dk. John Magufuli afanye kazi yake kwa kuwa amechaguliwa kihalali na bado hajamaliza hata kipindi cha kwanza cha uongozi wake.

Amewatahadharisha wananchi kuwa makini na wanasiasa kwa kuwa wapo baadhi wasio na nia njema na nchi badala yake wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi hata kama nchi inaweza kuingia kwenye majanga.

Pia amevitaka vyombo vinavyohusika na uratibu wa mambo ya siasa nchini hususan Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwatazama kwa macho mawili viongozi wa dini wanaotumia nyumba za dini kuwa majukwaa ya kisiasa huku wakiwayumbisha wananchi kwenye haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Aidha, ametaja sababu iliyomfanya ashindwe kulichukua jimbo la Vunjo ambapo pamoja na mambo mengine ni pamoja na hatua ya Rais Magufuli kumpigia debe jimboni humo jambo lililowafanya wamwonee donge na kuhamishia kampeni katika jimbo ili kuhakikisha halipati.

Hayo aliyasema jana mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam, alipokuwa akizungumzia hali ya kisiasa ya hapa nchini, ambapo alisema analaani kitendo cha wapinzani kudai Rais Magufuli hawatendei haki wananchi, anavunja sheria, katiba na anakiuka haki za binadamu na kuua demokrasia ya nchi.

Mrema alisema hivi sasa nchini kumeibuka vuguvugu la kisiasa hususan kwa wapinzani kutangaza serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. Magufuli imekuwa ikikiuka haki za binadamu na kuponda demokrasia jambo ambalo si la kweli kwa kuwa kila mwanasiasa yupo huru kuzungumza na kuchangia maendeleo kwa kadri anavyoweza.

Alisema wapo wanasiasa wanaodai Rais Magufuli hawatendei haki wananchi, anavunja sheria na kukiuka haki za binadamu huku wasemao hayo ndio vinara wakuu wa kukiuka haki hizo.

“Wapinzani wenzangu ndio vinara na waliokubuhu na vitendo vya kuaribu demokrasia nchini na kuwapotosha wananchi jinsi ya katiba inavyoenda nchini,”alisema Mrema.

Aliongeza kuwa kipindi cha uchaguzi mwaka jana, Mbunge wa Vunjo James Mbatia alikiuka sheria na maadili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015.

Mrema ambaye pia amewahi kuwa Mbunge wa Vunjo, alisema NEC na taasisi zingine zinazosimamia shughuli za kisiasa nchini zinapaswa kuwa makini na baadhi ya viongozi wa dini ambao wameacha jukumu lao kuu la kuwajenga kiroho waumini wao na kutumia vyombo vya dini kama kinga yao kwenye siasa.

“Wakati wa harakati za uchaguzi mkuu wa mwaka jana wapo viongozi wa dini waliosimama kwenye nyumba za ibada na kuwahubiria wafuasi wao kwamba mwaka huu rais lazima atoke kanda ya Kaskazini na nje ya hapo hatuwezi kukubali. Maneno hayo hayapaswi kuachwa yaendelee kwa kuwa ni hatari kwa mustakabbali wa siasa na maendeleo ya demokrasi hapa nchini.

“Wananchi kuweni makini si kila mwanasiasa anayekuja mbele yenu ana nia njema na taifa hili wengine lengo lao ni kutaka nchi iingie kwenye matatizo ili wao wanufaike,”alisema.

Akizungumzia kwa nini alikosa ubunge wa vunjo kupitia uchaguzi huo, alisema hilo lilitokana na mkakati wa wapinzani wenzake ambao walimuonea donge baada ya kuungwa mkono na Rais Magufuli aliposimama jimboni humo wakati wa kampeni na kumnadi.

“Nawashangaa wapinzani wenzangu hawajui kuwa Rais Dk. Magufuli anathamini zaidi mchango wangu nilioutoa nilipokuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, jinsi nilivyokuwa nafanya kazi kwa nguvu moja kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo,”alisema.

Aidha, Mrema alisema ana uhakika endapo Dk. Magufuli atakabidhiwa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), atamtafutia nafasi ya kumsaidia kushughulika na maendeleo ya Tanzania kwa kuwa kasi yake anaimudu na ataweza kwenda nae sawa.

Hivi karibuni vyama vya upinzani hususan vinavyounda UKAWA vimekuwa na kampeni ya kutaka kuzunguka nchi nzima kuishitaki serikali kwa madai imekuwa ikikandamiza haki hapa nchini.

Hata hivyo, tayari polisi imepiga marufuku mikutano, makongamano na maandamano yoyote ya kisiasa kwa kuwa yanamwelekeo wa kuwachochea wananchi kukiuka sheria za nchi na kushiriki matukio ya uvunjifu wa amani.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger