Mbunge huyo wa Kongwa aliondoka nchini Mei kwenda nchini humo, ikiwa ni takribani wiki mbili tangu kuanza kwa Mkutano wa Tatu wa Bunge la Bajeti ambao aliongoza vikao vichache, kipindi cha asubuhi, huku mchana akipokewa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema jana kuwa Ndugai alirejea nchini Julai 27 baada ya kukaa kwa zaidi ya mwezi mmoja akifanyiwa uchunguzi.
“Watanzania wasiwe na wasiwasi Spika amerudi na yupo katika afya njema. Maombi yao kwa Ndugai yalikuwa mengi na Mungu ameyasikia,” alisema Mwandumbya.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment