Aug 26, 2016

CCM Yaomboleza Vifo Vya Polisi Waliouawa Na Majambazi, Ole Sendeka Aivaa Chadema Kuhusu Maandamano ya UKUTA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Ndugu wanahabari,
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa sana taarifa ya kushambuliwa na kuuawa kwa askari wa jeshi la Polisi wakiwa katika kutekeleza majukumu yao ya ulinzi eneo la Mbande, Temeke jijini Dar Es Salaam.

CCM tayari imemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu pamoja na familia za marehemu waliofikwa na umauti katika tukio hilo baya katika historia ya nchi yetu.

Tunalaani tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuvipa ushirikiano wa kutosha vyombo vya dola ili kufanikisha wahusika wa tukio hilo kusakwa popote pale na kupatikana ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria haraka.

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi itaendelea  kuhakikisha amani ya Taifa letu inalindwa dhidi ya wachache wanaofurahia madhila kwa wananchi wetu. Wananchi wetu wanapenda, wamezoea na wanastahili amani. Ndio maana Tanzania imekuwa nchi ya kupigiwa mfano, ikionesha uongozi katika maeneo mengi. Tuendelee kuilinda taswira hii.

MAFANIKIO YA AWAMU YA TANO

Ndugu wanahabari,
CCM inachukua nafasi hii kumpongeza Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika muda mfupi wa uongozi wake.

Rais Magufuli aliahidi mabadiliko. Tunampongeza kwa kusimamia vema utekelezaji wa ilani ya CCM. Katika muda mfupi wa miezi tisa tu, Rais Dk Magufuli amefanya mambo makubwa.

Sote tunafahamu kuwa Shirika letu la Ndege, ATCL, limekuwa linafanya kazi na ndege moja. Serikali ya Dk Magufuli imekwisha lipia ndege tatu za abiria toka Canada, ndege mbili zitaingiza nchini mwezi ujao.

Reli ya kati inajengwa kwa kiwango cha Standard Gauge. Meli katika ziwa viktoria inanunuliwa ktk bajeti ya mwaka huu. Elimu ya msingi na sekondari inatolewa bure. Wanafunzi wetu sasa wanakalia madawati na kujifunza vizuri zaidi.

Barabara zimeendelea kujengwa. Makusanyo ya kodi yameongezeka. Huduma za jamii zinaendelea kuimarika. Lakini pia, nidhamu katika utumishi wa umma sasa imeimarika. Wananchi wanastahili huduma nzuri na kuthaminiwa na wafanyakazi wa Umma.

Mataifa mengi ya Afrika na nje ya Afrika yanaiga mbinu za Rais wetu katika kuleta mabadiliko nchini mwao. Hapa Kenya tu, Waziri mmoja wa Elimu anayesifika kwa utendaji kazi mzuri, anajiita “MAGUFULI.” Hata Australia, baadhi ya wananchi waliwahi kumtaka Waziri Mkuu wao afanye kazi kama Dk Magufuli.

Dk. Magufuli ameazimia kujenga uchumi wa viwanda. Ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa nchi yenye uchumi wa kati. Maisha ya wananchi wetu yataboreka.

Vijana wetu wapate ajira katika viwanda, watauza malighali na mahitaji mbalimbali ya viwanda. Wakulima watapata masoko ya bidhaa zao katika viwanda hivyo. Kilimo kitaongezeka thamani kutokana na mahitaji mbalimbali ya viwanda vyetu.  Hatua za kuelekea huko tayari zimechukuliwa.

Wapo wachache wanaelekea kutafuta mbinu chafu za kuhujumu mafanikio haya, lakini hawatafanikiwa. Watanzania wamemchagua Dk Magufuli ili awaletee maendeleo.

Serikali ya CCM, itawasaidia vijana wa Tanzania kuendesha uongozi wa Taifa lao. Kamwe tusikubali ndoto ya kuongoza mapinduzi haya makubwa kwa ajili ya Taifa na Bara letu ikapokonywa na watu wachache wasiokuwa na dira ya kuliletea maendeleo Taifa letu. Tuwapuuze.

UPINZANI KUSUSIA VIKAO VYA BUNGE

Ndugu Wanahabari,
Bunge kama ilivyo kwa mhimili mingine linaongozwa kwa katiba, sheria na kanuni katika mijadala na maamuzi yake. Kama Mbunge hajaridhika na maamuzi ya Spika, Naibu Spika au Mwenyeki wa kikao, kuna taratibu za kufuata. Utaratibu wa kikanuni ni kuulalamikia uamuzi huo kwa Katibu wa Bunge.

Wakiwa wanafahamu taratibu za kikanuni, kama kawaida yao, WAPINZANI, waliamua kuzisigina na badala yake wakataka Naibu Spika aondolewe.

Hivyo wakaratibu kupigwa kura ya kutokuwa na imani na Naibu Spika. Ambapo suala hilo lilipelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Kutokana na kutokuwepo kwa Spika nchini, hoja hiyo haikufikia ukomo. Tunamshukuru Mungu afya ya Spika imeimarika. Sasa hoja hiyo huenda itafikishwa katika mkutano wa Bunge litakalokaa mwezi ujao.

Kana kwamba hiyo haitoshi, kama kawaida yao, hawakuwa na subira ya kufuata taratibu. Wakaamua kufanya kihoja. Wakaamua kutohudhuria vikao vyote vya Bunge vilivyokuwa vikiongozwa na Naibu Spika.

Na hata walipoingia Bungeni waliziba midomo yao na kuamua kutowasalimia wabunge wenzao wa CCM, kutopeana mikono na hata kutohudhuria misiba na sherehe zao.

Vitendo vyao hivi ndivyo vimeasisi chuki ndani ya jamii yetu iliyozoea UPENDO, UDUGU, UMOJA NA MSHIKAMANO. Watanzania tunafahamika na tunaona fahari kuishi kama ndugu.

Baada ya kitendo hicho cha kuwasaliti wapigakura wao kulaaniwa kila kona ya nchi, sasa wamekubali kutumiwa kama vibaraka kuichafua taswira ya nchi yetu, nao kwa hila iliyo wazi, wamekubali kuwafitinisha watanzania kwa kuandaa maandamano ya nchi nzima, yasiyo na ukomo. Hatua hii ni uvunjaji wa katiba ya nchi, Sheria na inalenga kuvunja amani, utulivu na mshikamano wa watu wetu.

Ileleweke kwamba, wanachokifanya hawa CHADEMA ni kuchochea wananchi kwa makusudi kutotii maagizo halali ya vyombo vya dola na Serikali kwa visingizio mufilisi kuwa katika Katiba imewapa uhuru huo. Katika haitoi haki na uhuru usio na ukomo. Ibara ya 29 (5) inasema;

 “Ila watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vinavyotajwa na katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma”

Baada ya kusema hayo, ninaomba CHADEMA wakumbuke na kutilia maanani kuwa kila haki ina wajibu na hakuna haki au uhuru usiokuwa na ukomo hususani pale inaposababisha kuingiliwa ama kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine. Rejea ibara ya 30 (1) na (2) ya Katiba.

Ndugu wahabahari,
Mwisho tunatoa pole kwa wenzetu wa CUF kutokana na mapambano huko kwao. Tumestushwa sana na yanayoendelea huko. CCM inawapa pole na tunawatakia maelewano ili waje tusaidiane kuwaletea watanzania maendeleo.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.


Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger