John Cheyo |
Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na Chama cha Demokrasia (CHADEMA).
Cheyo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.
“Watanzania wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.
Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi.
Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.
Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.
Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi lolote.
Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment