Unakuta mwanaume kasoma hadi chuo, form six n.k lakini hajishughulishi kwa lolote anaishi kwao, kwa ndugu, kwa marafiki kajipiga sopusopu tu na ana afya njema anacheka hadi jino la mwisho hashtuki kimbia umelamba dume!
Hebu jiulize mwanaume ambaye hajiwezi yeye mwenyewe unategemea akupe msaada gani katika kulea watoto endapo mtaoana? analishwa, kodi hajui kuisotea hajui kukuru kakara za wenye nyumba unategemea atawaza kujenga? sahau!
Utamkuta busy kuponda kazi za wenzake na kuziona ni mbaya ni za hali ya chini yeye ndo mjanja hafanyi kazi za kifala, anajisemea kikazi cha laki 3 sifanyi huku akiambiwa asimamie show ya tumbo lake tu semister moja anachemka!
Hivi hadi vibarua vya kawaida hawezi kufanya akapata chochote walau akawa na maisha yake ya chini ya kuanzia, kubeba zege, mbogamboga, matunda n.k hawezi kuuza?
Kiufupi ukiona mtu mzima ni tegemezi usitegemee mazuri wana tabia hizi:
- Hawajiamini(ugomvi kila mara)
- Huwa wababe sana walau
- Huonesha uanaume wao
- Hawana shukurani hata wafanyiqe nini kulalamika tu.
- Hawawakubali watu wengine huponda kila kitu.
- Hata akikosea haombi msamaha anahisi samahani ni umasikini
- Mkihitilafiana kidogo huunganisha na umasikini wake labda ndo maana mnagombana!
- Hana tabia maalum akipata ka elf hamsini hilo gubu lake ni hatari
- Kama ni mchumba akipata hela lazima akuache maana anahisi kwakuwa unajua historia yake hutamthamin (hawajiamini)
Kama unabisha Toa Maoni yako Hapa Chini Kwa Hoja....
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment