Naibu Spika Tulia |
naibu spika
Akizungumza hayo katika mahojiano maalumu katika kipindi cha DAKIKA 45, kinachorushwa na kituo cha ITV, Dkt Tulia alisema makundi yote ya wabunge yakishaapishwa wote ni wabunge wanaofanana katika hadhi ya kufanya kazi wanapokuwa Bungeni.
“Katiba ilivyoyaweka makundi matano ya wabunge kuanzia wanaoteuliwa na Rais, wanaochaguliwa na wananchi, wabunge wa viti maalum na wanaotoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wote wamewekwa kwa sababu maalumu kwa sababu hiyo wabunge wote ni sawa,” alisema Dkt. Tulia
Aidha Naibu Spika huyo ameitaka jamii kubadilika kutoka katika dhana kwamba mwanamke ambaye anashika nafasi ya juu katika uongozi kwamba amebebwa.
“Wanawake wengi ambao wamepewa nafasi ya uongozi kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni mara chache sana hufanya vibaya na hata akifanya vibaya jamii humhukumu kwa kuwa ni mwanamke wakati kuna wanaume katika nafasi kama hiyo ambao pia unakuta wamefanya vibaya hivyo kuna changamoto hiyo katika jamii,” alisisitiza.
Kwa upande mwingine aliweza kuelezea utendaji wake wa kazi tangu alipoanza kwa kusema, “nimeongoza Bunge bila upendeleo wowote ila nafuata sheria na kanuni za kuongoza Bunge na pia katiba inawatambua Wabunge wote wapo sawa.”
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment