Profesa Ibrahim Haruna Lipumba katika utetezi wa hoja yake ya kujivua madaraka ndani ya CUF alisema kuwa NAFSI IMEMSUTA kwa yeye kama mwenye kiti wa chama kumpokea mtu ambaye siyo msafi katika umoja wao wa UKAWA kipindi kile. Kutokana na hilo Haruna akaamua kujiudhuru uenyekiti wa chama na kutuacha angani tukiwa tunaelea bila rubani.
Kwa sasa hali imetulia na ndege ipo kwenye mstari, anarudi na anatueleza kirahisi kabisa kuwa ametengua barua yake ya kujiudhuru na sisi tulivyo na akili fupi tunashangilia na kumuona kama mkombozi wa chama.
Labda niwakumbushe wana CUF wenzangu: kwa miaka takribani ishirini hatukuwahi kuwa na wabunge hata watatu wa kuchaguliwa Tanzania bara tukiwa na Haruna. Haruna ameondoka tumepata zaidi ya wabunge watano Tanzania Bara huku chama kikijijengea heshima kubwa.
My take:
Wana CUF tuamke siku tutakayokuja kumgundua Haruna, tutakuwa tumeshachelewa.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment