Aug 8, 2016

Maneno ya Haji Manara katika kutimiza miaka 80 ya Simba leo


Watanzania wenzangu hususan wana Simba, tarehe kama ya leo 8-8-1936, wazee wetu ambao wengi wao tayari wapo mbele ya haki.walianzisha klabu yetu hii ambayo leo tunaishangilia na kuipenda sana.

Klabu hii ndio klabu bora ya karne kwa ukanda wa afrika mashariki na kati ikiwa na rekodi isiyoguswa kwa kutwaa mara nyingi zaid ubingwa wa wa vilabu kwa kanda yetu hii,sambamba na kuwa klabu yenye rekodi bora zaid kwa vilabu vya Tanzania,nje ya mipaka ya nchi yetu.

Wanasimba nnajua wengine watajisikia vbaya kwa mm kuwakumbusha huo ukweli,ila hiyo ni 'fact'isiyohitaji shule kubwa kuijua.kwa vigezo vyovyote vile vinavyokubalika na FIFA na CAF.Simba ndio timu bora ya muda wote kwenye zone yetu hii.

Tujivunie ukweli huu na tutembee kifua mbele.

Wanaotupinga hujadili miaka minne ya nyuma ambayo sote tunajua hatujafanya vizuri,lakini niwaambie wanakosea mno, ktk miaka minne iliopita ukuaji wa uchumi kwa taifa la Marekani huwezi kulinganisha na China.
Sasa kiakili.utalinganisha Marekani na China kwa ukubwa wa taifa?

Lipi taifa kubwa kati ya USA na China kwa vigezo vya taifa imara.kiuchumi,kiulinzi, kisiasa na kiutamaduni? 
Sisi ni mfano wa Marekani na wao ni mfano wa China.mbingu na ardhi.na ndio maana jina letu maarufu ni Simba TAIFA KUBWA.

Najua miaka hii themanini tumepitia changamoto nyingi sana ambazo nyingine si nzuri hata kidogo, lakini siijui klabu yenye umri kama wetu duniani isiyopitia maswahibu kama yetu.

Moja ya changamoto kubwa tulio nayo ni kutojitegemea kama klabu na kutokuwa na uwanja wake wa mazoezi wenye hadhi ya TAIFA KUBWA.

Kwa sasa hili la uwanja uongozi wenu unaongozwa na Rais Evans Aveva umeamua kulivalia njuga,hivi nnavyoandika ujumbe huu, mkandarasi yupo SITE tayari.ujenzi wa uwanja wa mazoezi unajengwa na ndani ya majuma machache yajayo.jiwe rasmi la msingi litawekwa na ndani ya msimu huu tutaanza kuutumia.

Uwanja huu utakuwa ni wa nyasi bandia na pia utakuwa na hosteli ya kuishi wachezaji wetu wanapookuwa kambini na huduma muhimu zinazopsswa kuwepo kwenye kambi ya klabu yenye hadhi kama ya Simba,
Ieleweke kwa sasa.kipaumbele ni kuanza na sehemu ya kuchezea,ambayo inatutafuna mamilioni ya shilingi kwa kukodisha viwanja vya kufanyia mazoezi.

Kuhusu kutokujitegemea kwa klabu, huu ndio mzigo mzito tulio nao kwa sasa.kwa miaka yote.Simba inaendeshwa kwa kutegemea wafadhili na kwa miaka ya karibuni na wadhamini wetu.huku mapato ya mlangoni yakiwa ndio chanzo kikuu cha mapato kinachoendesha klabu,sambamba na sehemu tulizopangisha kwenye majengo yetu yaliyopo mtaa Msimbazi jijini Dar es salaam.

Huku pia tukipata 'kiduchu'sana toka kwa wanachama wetu kama ada ambao baadhi yao nao hutegemea ufadhili wa kulipiwa ada hasa inapofika wakati wa uchaguzi mkuu wa klabu.

Kwa mapato na vyanzo hivyo.ni wazi sasa lazma tutoke hapo, ni lazma tubadilishe fikra zetu kwa Simba mpya.hatuwezi kuwa na muundo huu tena baada ya kuishi nao kwa miaka themanini.

Rai yangu kwa wanachama na wapenzi wa Simba, kwa kuwa uongozi wetu nao unaafiki mabadiliko ya kimuundo mpya.sote tushirikiane kuleta Simba mpya.
Haitapendeza ktk kipindi hiki kulumbana mitandaoni au kwenye vyombo vya habari kwa kisingizio cha mabadiliko.mabadiko yaje huku tukiwa wamoja.

Yaje huku tukiwa na mawazo huru.yaje huku tukiwa tunajua sisi sote tutakuja kuandikwa kwenye historia ya klabu yetu.kuwa kizazi flani kilileta mabadiliko ya kimuundo.lakini kubwa yaje huku tukirejeshe heshma ya klabu ambayo imeyumba ktk miaka minne ya nyuma.

Simba mwaka huu licha ya kutaka mabadiliko.kipaumbele chake kikuu ni vikombe, na ndio raha na furaha ya mwanasimba, uongozi,wanachama,wachezaji na benchi lao la ufundi na washabiki wote.lazma tuwe wamoja.tuondoe chochote kile kitakachotugawa.sisi ni wamoja kiasili na ndio maana kaulimbiu yetu inasema hvyo.umoja wetu hauthaminishwi na chochote kile.

Wenzetu kwa bahati mbaya unaunganishwa na kitu, sisi umoja wetu ni wa damu na unaandikwa kikatiba. Tusifarakane hata kidogo kwenye kipindi hiki.tuwe na subira na hayo mabadiko na uongozi naamini kwa uharaka utatekeleza maamuzi ya mkutano mkuu wa 31-7-2016.

Niwaombe sana wanasimba wenzangu.ujaji wa badiliko lolote kubwa lazma liende sawia na fikra pevu zitakozoelewa nn tunataka kwa Simba ijayo.

Tusikurupuke kwa jazba au mihemko na tukifanya hvyo tutakuja 'kuazimwa'kama dera la kwendea harusini.tujiongeze hssa nn tunataka.huku tukipokea elimu pana ya mifumo ya uendeshaji wa vilabu vilivyofanikkwa zaid afrika na duniani kwa ujumla.

Nasisitiza muundo wowote tutakaochagua.uwe wa hisa au mwingineo, lazma tuujue vzuri faida na hssara zake.na hapa uongozi hatuna budi kuandaa utaratibu wa kuelimisha watu wetu kuepukwa na sisi  'kuazimwa'

Mwisho niwaombe sana mliopo jijini na mikoa ya jirani tuje uwanja wa taifa mchana huu kuadhimisha miaka themanini ya klabu yetu. Pia leo ni kilele cha wiki yetu inayotuingiza kwenye msimu mpya.

Jioni ya leo tutajua sura ya timu yetu msimu ujao wa ligi. Njooni mumshangilie mnyama.njoon tuujaze uwanja.njooni tuonyeshe tofauti yao na sisi.

Mungu ibariki Simba

Mungu ibariki Tanzania


Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger