Aug 15, 2016

Ndoa za Mastaa wa Bongo Zilizoota Mbawa

MAISHA ya kiuhusiano kwa mastaa ulimwenguni kote ni ya tofauti sana na watu wengine wa kawaida ambao hawana majina katika jamii zao.

Mara nyingi maisha yao yanakuwa ya kuangaliwa sana na watu, hasa juu ya namna gani watakuwa wamefanya vitu vipya kila siku.

Jambo la kushangaza, ukiwafuatilia baadhi ya mastaa, maisha yao kabla ya kuwa na majina yalikuwa tofauti kabisa.

Hata hivyo, mara nyingi mastaa hujikuta wakilazimika kuishi maisha ya kuigiza. Utakuta mbele za watu wanaonyeshana mapenzi mazito, lakini ndani kuna chokochoko za hapa na pale na si ajabu moto mkubwa unawaka.

Ilivyo ni kwamba, mastaa wengi hushindwa kudumu kwenye uhusiano kwa muda mrefu, huku kukiwa na mtindo wa cheni, kwa maana ya msanii mmoja wa fani fulani, kuachana na mwenzi wake kisha kwenda kwa mwingine.

Hata wale wanaobahatika kuingia kwenye ndoa, mwanzoni huwa na cherekochereko na furaha, lakini baada ya muda, utasikia fulani kaachana na fulani. Wengi wanaoulizwa, huishia kuwalaumu wenzao huku wakitaja sababu mbalimbali.

Kuna listi ndefu ya mastaa walioanzisha uhusiano na kutemana baada ya muda, lakini hapa nakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao walifanikiwa kuingia kwenye ndoa, baadaye wakatofautiana na kutengana kwa sababu mbalimbali.

 AUNT EZEKIEL

Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel alifunga ndoa na Mbongo aishie Dubai, Sunday Demonte, Oktoba 18, 2012. Katika ndoa hiyo, Demonte aliwakilishwa na rafiki yake, kisha sherehe ya nguvu ilifanyika baadaye Dubai.

Hata hivyo, miezi kadhaa baadaye ndoa hiyo ilianza kupoteza muelekeo hasa baada ya Aunt kuonekana Bongo muda mwingi kuliko nyumbani kwake Dubai, lakini baadaye ikathibitika wazi kuwa wamemwagana.

Kuachana kwao siyo siri, kwani Aunt alianzisha uhusiano na densa wa Diamond aitwaye Mose Iyobo. Kwa sasa msanii huyo ni mjamzito, ambao hajamtaja mhusika wake.

IRENE UWOYA

Jumamosi, Julai 11, 2009, staa wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya alifunga ndoa na msakata kabumbu, Hamad Ndikumana katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Baada ya ndoa hiyo, sherehe yenye hadhi ilifanyika kwenye Hoteli ya Giraffe View, Mbezi – Kawe, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo mastaa mbalimbali.

Ndikumana Raia wa Rwanda, wakati akifunga ndoa na Irene,  alikuwa akiishi jijini Nicosia, Cyprus ambapo alikuwa akicheza mpira katika Klabu ya AEL Limassol na baadaye Apop Kinyras Peyias FC.

Baada ya ndoa yake, aliongozana na Irene hadi huko na kuanza maisha yao ya ndoa. Hata hivyo, ndoa hiyo ilivunjika Novemba, 2011 baada ya Irene mwenyewe kukiri kuwa amekuwa akiishi na Ndikumana kwa mazoea tu, lakini moyoni hakuwa akimpenda!

JACK PATRICK

Modo Jacqueline Patrick ambaye kwa sasa yupo nyuma ya nondo, nchini China kwa madai ya kukutwa na madawa ya  kulevya, Desemba, 2011 alifunga ndoa na Abdulatif Fundikira katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Ndoa ya wawili hao haikudumu muda mrefu, kwani baadaye mwaka 2012 ilivunjika. Hilo lilithibitika hasa pale Jack alipoanzisha uhusiano mwingine usio wa siri na msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid  ‘Jux’.

Kwa sasa yupo gerezani huko Hong Kong, China katika Mji wa Macau akikabiliwa na madai ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin aliyokamatwa nayo Desemba 19, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Macau. Alikuwa akitokea jijini Bangkok, Thailand akielekea mjini  Guangzhou, China.

JAYDEE

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jaydee’ na mtangazaji Gadner G. Habash walifunga ndoa Jumamosi, Mei 14, 2005 jijini Dar es Salaam hadi ilipovunjika katikati ya mwaka juzi.

Kwa sasa kila mmoja anaishi kivyake. Hivi karibuni Garder akiwa jukwaani alitamka maneno yenye viashiria vibaya yakionekana kumlenga Jaydee lakini hakuna aliyethibitisha.

Kwa upande wake Jide, hakuwahi kujibu hilo hata alipotakiwa hivyo na waandishi mbalimbali kwa nyakati tofauti.

DIDA

Huyu ndiye fungakazi. Ni rahisi kusema ndiye staa aliyeingia kwenye ndoa na kuvunjika mara nyingi zaidi kuliko wote. Ni mtangazaji Hadija Shaibu ‘Dida’ aliyeolewa na Ezden Jumanne mwaka 2013 na kuachwa kwa talaka Juni, mwaka jana, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya ndoa hiyo.

Kabla ya Ezden, Dida aliishi na Gervas Mbwiga ‘G’ kwa ndoa kabla ya kuachwa kwa talaka mwanzoni mwa mwaka 2013 akiwa amefunga ndoa hiyo mwaka 2011.

Mume wa kwanza wa Dida alikuwa ni Mohamed Mchopanga ‘Mchops’, ambaye ndiye aliyesababisha akapewa jina la Dida wa Mchops enzi hizo za mapenzi yao.

NORA

Mume wake wa kwanza alikuwa ni marehemu William Limbe ‘Ng’wizukulu Jilala’. Kabla hajafariki alimpa talaka  mwaka 2010, ambapo baadaye Julai 1, 2010 mwigizaji huyu, Nuru Nassor ‘Nora’ aliolewa tena na Masoud Ally ‘Luqman’ lakini ikavunjika mwishoni mwa mwaka 2012.

HUSNA MAULID

Ndoa ya mshiriki wa Miss Tanzania, 2012, Husna Maulid na mumewe aliyetajwa kwa jina moja la Abou nayo ilivunjika miezi michache baada ya kuoana.

Mtanzania

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger