Akiandika katika ukurasa wake wa Facebook jana, Kibatala alisema: “Tunasikitika nawe, na kukupa pole nyingi sana.”
Katika ujumbe huo aliothibitisha baadaye kuuandika, Kibatala aliongeza: “Tunakushukuru sana kwa kutoa ushahidi wa ukweli na wa haki katika kesi za uchaguzi majimbo ya Kilombero na Mlimba yaliyotolewa hukumu jana (Julai 29).”
Wakili hiyo aliongeza: “Wakati wa Uchaguzi Mkuu ulikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero na Msimamizi wa Uchaguzi katika Majimbo waliyoshinda Chadema.”
Juzi, taarifa ya Ofisi ya Rais–Tamisemi iliyotolewa na Katibu Mkuu, Mussa Iyombe bila kufafanua sababu za kuenguliwa kwake, ilieleza kwamba Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mbilinyi kwa sababu hakuridhishwa na utendaji wake wa kazi.
Mbilinyi alikuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilombero kabla ya kuhamishiwa Dodoma na baadaye Bagamoyo.
Alipotafutwa kuthibitisha maneno yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa facebook, Kibatala alisema: “Ni kweli niliandika kwenye ukurasa wangu wa facebook na ninaomba maneno hayo yabaki kama yalivyo, naona watu wengine wameanza kutafsiri vinginevyo.”
Katika hukumu hizo, Majaji Projest Rugazia na Penterine Kente waliwapa ushindi wabunge wawili wa Chadema, Susan Kiwanga na Peter Liajualikali baada ya kukosekana ushahidi wa kutengua matokeo hayo.
Juhudi za kumtafuta Mbilinyi kuzungumzia hatua iliyochukuliwa dhidi yake hazikuzaa matunda kutokana na simu zake zilizopigwa mara nyingi kutokuwa hewani.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment