Wadadisi wa mambo ya kisiasa nchini waazitataja siasa za nchi hii kama siasa uchwara zisizo na misimamo ambazo hutawaliwa zaidi na "mahitaji ya tumbo", kuliko uzalendo wa kujitoa kulitumikia Taifa.Hizi ni siasa maslahi ambazo badala ya kujikita katika itikadi na falsafa za vyama, zinaongozwa na njaa za wanasiasa uchwara waliotayari kuvisariti viapo vyao kukidhi mahitaji ya matumbo yao. Matokeo ya wanasiasa wa aina hii ni kuwakatisha tamaa wanamabadiliko wa kweli waliojitoa muhanga kulitoa Taifa letu katika utawala dharimu wa CCM.
Mara nyingi tumekuwa tukijiuliza,inakuwaje mtu tuliyemuamini kuwa amejitoa kwa dhati kulipigania Taifa kupitia siasa za mageuzi,afike mahali arudi nyuma na kuyarudia matapishi yake huku akisahau majina aliyoitwa majina kama " oil chafu na mengineyo" wakati alipojiondoa CCM na kuja upinzani?
Jibu la maswali haya nimelipata jana hapa Kahama katika mkutano wa hadhara wa JPM uliofanyika katika viwanja vya milango kumi hapa Kahama maarufu kama "uwanja wa Magufuli". Katika mkutano huo nilishuhudia nguvu kubwa ya ushawishi aliyoifanya JPM akimshawishi aliyekuwa mbunge wa Kahama na mgombea ubunge kupitia CHADEMA 2015 James Lembeli alejee CCM.Umma wa wakazi wa KAHAMA ulipigwa na butwaa na kutoamini namna Rais alivyokuwa anatumia madaraka yake kumshaeishi James Lembeli arejee CCM kwa ahadi kemkem.
Msikilize Magufuli katika video hii akimshawishi Lembeli arudi CCM
Jambo la msingi tunalopaswa kujiuliza: ikiwa Rais alitumia ushawishi wa kiwango hiki hadharani mbele ya mkutano wa hadhara kumuomba Lembeli arejee CCM, ni nguvu gani ya ushawishi hufanywa sirini kuwarubuni makamanda wetu waviasi vyama vyao na kurejea CCM?Unafikiri ushawishi ule alioufanya JPM akimuomba Lembeli arejee CCM ulianzia pale mkutanoni katika viwanja vya Magufuli?Jibu ni kwamba alichokuwa anakifanya JPM pale mkutanoni ni mwendelezo wa juhudi za chini kwa chini anazozifanya na zifanywazo na wenzake kuwarubuni viongozi na wanachama wa upinzani kurudi CCM.
Ni dhahiri kuwa upinzani kunahitaji moyo,ni wachache sana wanaoweza kukataa " ushawishi wa Rais"wa kujiunga na CCM, kwa siasa zetu zinazoongozwa na tumbo, ni nadra kwa mtu mwenye njaa kuukataa wito wa rais,rais mwenye mamlaka za uteuzi na anayeweza kukuteua na kukupa uraji wa kukidhi njaa ya tumbo lako. Inahitaji ujasiri wa kikamanda na moyo wa kizalendo kuvishinda vishawishi vya rais na nguvu ya fedha na ahadi za vyeo ili usirejee ccm,vinginevyo hakuna awezaye kushindana na ushawishi wa aina ile nilioushuhudia jana hapa Kahama.
Shukrani kwa Lembeli kwa "kusita" kutimiza makubaliano ambayo naamini tayari yalikuwa yameshafikiwa kabla ya ule mkutano,lakini nilichokishuhudia pale tayari "roho ya usariti" imeshauingia moyo wa Lembeli,kinachosubiriwa ni muda muafaka tu ili aandaliwe mkutano mwingine wa kumpokea akirejea tena CCM.Pale mkutanoni alisita kutimiza "usariti" wake,lakini alimuhakikishia JPM kuwa "mkia wake bado upo" na anasubiri kutekelezwa kwa mambo flaniflani ili ayarudie matapishi yake kwa kurejea tena CCM.
Njaa ni jambo la kawaida kwa viumbe hai,lakini njaa hugeuka kuwa mbaya pale inapohama toka tumboni na kuingia kichwani. Lembeli huyu huyu aliyeuaminisha Umma wa wanakahama kuwa alishauriwa na mama yake (Mwana Maria) na mizimu ya kwao ilimpa baraka atoke CCM na kujiunga UKAWA, leo anaisariti hadi mizimu yake anayoiamini? Njaa mbaya jamani!!!
Wapenda mabadiliko tusikatishwe tamaa na makamanda waasi wanaoikimbia kambi kwa ushawishi upitao akili zao,ila jambo lililodhahiri ni kwamba,wote wanaorejea CCM hufanya hivyo baada ya vikao vya muda mrefu vya ushawishi vifanywavyo na ccm na serikali yake,wanachokifanya jukwaani mbele za watu ni hatua ya mwisho tu ya kukamirisha usariti wao baada ya mhusika kutimiziwa daadhi ya ahadi alizoahidiwa.
Imeandikwa na ZILLAHENDER MPEMA/Jamii Forums
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment