Hamad Rashid |
Swali; unadhani nini kimejificha nyuma ya mgogoro wa CUF?
Jibu: CUF imeondoka katika muundo wa kuwa taasisi na kimekuwa chama kinachoongozwa na mtyu mmoja anayeshirikiana na watu wawili au watatutu wanaomuunga mkono. Ikiwa watu wanaanzisha chama kinachoamini katika muungano halafu anajitokeza mtu mmoja anasema anataka muungano wa mkataba, hapa kuna tatizo. Ugomvi CUF utaendelea kwa sababu kuna sultani anyetaka kusikilizwa kila anachotaka kifanyike bila kujali kina manufaa gani kwa chama.
Kwa mfano mimi nilishutumiwa kwamba nimetaka kugombea ukatibu mkuu ili nimpiku Maalim Seif.
Swali: Kuna sababu nyingine iliyokufanya ufukuzwe CUF?
Jibu: Walinizushia nimepewa fedha na Pengo (Kardinali), Pinda (aliyekuwa waziri Mkuu) na Lowassa (aliyekuwa mgombea wa UKAWA) ambaye wamemchukuwa na kufanya naye siasa kila mahala.
Swali: Unashauri Lipumba na Seif wafanye nini ili wamalize mgogoro?
Jibu: Kama hawataki kukaa na kuangalia katiba ya chama bila kumuangalia mtu usoni watateketea.
Swali; Kwa nini CCM hakuna migogoro mingi kama wapinzani?
Jibu: CCM wana madhambi yao, lakini wameweka utaratibu wa kuheshimu chama, lakini CUF wanafukuza watu kwa sababu haiendeshi kitaasisi.
Swali: Lakini kuna madai kuwa wewe unatumika na CCM?
Jibu: Sishangai kusikia hivyo, kwa kuwa hao wanaoniambia natumika na CCM walinishutumu natumika na Chadema nilipokuwa kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni. Nilishazoea kushutumiwa ila tofauti yangu na wao ni kwamba mimi siwezi kutumia lugha ya matusi katika kuwajibu.
Swali: Kuna watu wanaamini kuwa ni tabia ya Seif anapomchoka mtu (mwenyekiti) anamtengenezea zengwe . Wakitolea mfano wa wenyeviti wastaafu kama Mapalala. weweuna maoni gani?
Jibu: Ni kweli Mzee Mloo alisema anataka apumzike, lakini baadaye akaona aendelee na akapita kwa Katibu Mkuu (Seif) na alimkubalia,ila baadaye yakatengenezwa kuwa kauli yake aliyoitoa awali iwe hiyo hiyo, hakuangalia kwamba ni mtu ambaye amejitolea kwenye chama. Kama kuna watu walijitoa sana katika chama wakadhalilishwa na kufukuzwa, sasa hiki kinachoitafuna CUF ni dhambi ya ubaguzi na ubinafsi.
Swali: Unadhani nani kakosea kati ya Lipumba na Seif?
Jibu: Naona wote walikosea kwa namna walivyojiunga na Ukawa. Hawakuangalia madhara yanayoweza kukipata chama. Uamuzi ule haukuwa na Baraka za mkutano mkuu wa chama. Ilikuwa ni lazima mkutano mkuu wa CUF ukubali kwanza kwamba watasimamisha mgombea uraisi kabla ya kujiunga na Ukawa, lakini wao walijiamulia kirafiki rafiki. Chadema walikuwa wajanja walienda katika mkutano mkuu kuomba Baraka na wakawazidi ujanja wengine kwa kulazimisha kumpitisha Lowassa.
Swali: Unadhani ni kwanini Lipumba na Seif hawakushitukia njama hizo?
Jibu: Kwa sababu Chadema walisema hawatasimamisha mgombea Zanzibar, Maalimi Seif aliwakubalia ili akagombee uraisi huko na aliona hilo lingefanikisha malengo yake.
Swali: Kuna maoni tofauti kuhusu uamuzi wa Msajili dhidi ya mgogoro huo wa CUF.
Jibu: Msajili alikuwa sahihi kwa kuwa alizingatia katiba ya CUF inavyosema. Halupendelea upande wowote. Ukiisoma katiba ya CUF hata wewe ambaye siyo mwanasheria utakuwa upande wa Msajili.
Swali: Kwa mgogoro uliopo nini inaweza kuwa hatima ya CUF?
Jibu: Naona CUF ikimfia Maalim Seif.
Swali: Unaionaje CUF ndani ya Ukawa?
Jibu: CUF imemezwa na Ukawa. Haiwezi kuendesha siasa ikiwa ndani ya umoja huo wa vyama vine.
Swali: Unaweza kutofautishaje mgogoro kati ya Seif na Lipumba na ule wa kati yako na Seif hata ukatimuliwa na kuamua kuunda chama kingine (ADC)?
Jibu: tofauti ni kuwa stori zetu zilivyotengenezwa tulitakiwa tupate tafsiri ya kisheria zaidi lakini mgogoro wa sasa unaendeshwa na siasa.
Suala letu lilipata Baraka kwa wanachama wengi wa CUF waliamini tuna makosa hadi sasa ndio wanaotutafuta kutuomba radhi tofauti na sasa ambapo watu wengi wa Zanzibar na Bara wanamuunga mkono Lipumba.
Nimewasilisha kama ilivyo;
Ila inavyoonyesha mgogoro ndani ya CUF ni tofauti na watu wanavyopelekeshwa na upepo wa kisiasa....tunaomba hoja kwa hoja, mahojiano haya ayapate Seif,Mtatiro na wenzake ili watolee ufafanuzi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment