Askofu Mameo ameyasema hayo katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika jana katika usharika wa Kijitonyama Jijini Dar es Salaam ambapo siku hiyo ilikuwa maalumu kwa watoto.
“Siku hizi kuna hii mitandao ya whatsapp, twitter, na facebook imefanya wazazi wanakuwa bize kuchati na kuangalia video na picha na kusahau wajibu wao wa kuwalea watoto katika njia inayofaa katika jamii na yenye kumpendeza Mungu.
Askofu Mameo ameongeza kuwa taifa lolote msingi wake ni watoto na kama jamii ikikosea katika msingi huo ndiyo maana siku hizi watoto wanapewa majina ya ajabu kama vile panya rodi, chokoraa jambo ambalo halimpendezi Mungu.
“Wazazi tuna wajibu wa kuwalea hawa watoto, kuwa karibu nao na kujua kama wanakwenda shule kweli au wanaishia kwenye vibanda vya kucheza michezo ya ajabu na pia kuchunguza makundi wanayocheza nayo kama yanaeleweka kimaadili au la” Amesema Askofu Mameo.
Aidha pamoja na hayo Askofu Mameo ameenda mbali na kutoa mifano ya kiutendaji katika taasisi za umma kwamba kama watoto hawataandaliwa vizuri hata wakipata kazi wanakuwa hawana heshma na maadili katika kazi zao.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment