Serikali haitajiondoa katika Mahakama ya ICC licha ya kwamba baadhi ya nchi barani Afrika zimeonesha nia ya kujitoa na kutokua na imani na utendaji kazi wa mahakama hiyo. "Mpaka sasa hakuna sababu ya kujiondoa katika mahakama hiyo kwa kuwa nchi haijafika mahali ambapo kuna watu au vikundi vya watu ambao wamehusika na makosa ya jinai, makosa ya kimbari, makosa dhidi ya binadamu au makosa ya kivita. Alisema Waziri Mahiga
Amesema Tanzania haijaombwa kuunga mkono swala la kujitoa katika mahakama hiyo kwakuwa kulikuwa na mjadala wa nchi za Umoja wa Afrika zijiondoe kwa pamoja katika mahakama hiyo kwa umoja lakini hakukuwa na makubaliano wala muafaka wa jambo hilo hivyo hakuna sababu ya kujitoa katika mahakam hiyo.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment