Akizungumza katika kongamano la kupinga adhabu ya kifo lililofanyika jijini Dar es Salaam,mkurugenzi wa sheria na kituo cha haki za binadamu,LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alisema, “Kwa sisi tunavyoamini kwa haki za binadamu ni adhabu inayopoteza utu wa mtu lakini ni adhabu ambayo haisaidii yule aliyefanya kosa kuweza kujirudi.”
“Lakini ni adhabu ambayo pia ikikosewa hauwezi kubadilisha. Kwahiyo kwa adhabu kama hiyo inabidi tujiangalie mara mbili kabla ya kukubali kuendana nayo,” aliongeza.
Alisema kuwa nyingi zimeshafuta adhabu hiyo zikiwemo 20 za Afrika na hivyo Tanzania haina budi kufanya hivyo pia.
Kongamano hilo lilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini, viongozi wa dini na wadau mbalimbali
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment