Meneja wa TRA mkoa wa Mara, ERNEST NKANGAZA ameiambia ITV kuwa bidhaa hizo zikiwemo galoni zenye mafuta ya taa Lita zaidi ya 2,725,Diseli Lita 960, Mifuko ya Plastiki ambayo imepigwa marufuku kuingizwa nchini pamoja Pipi na Dawa za Binadamu ambazo zimekamatwa katika kijiji cha Maburi wilayani Serengeti.
Amesema maafisa wa TRA walipata taarifa kuhusu gari yenye namba za usajili T881 BDE ambayo imeandikwa ubavuni AMOS .J. BUHEMBWE ikiwa imebeba bidhaa hizo na waliweka mtego katika makutano ya Barabara ya Makutano ya Musoma-Mwanza na saa saba usiku gari hilo lilipofika eneo hilo na dereva wake aliamuliwa kusimama na kukaidi na kuliondoa kwa mwendo kasi hivyo kufukuzana hadi kijiji cha Maburi walipolitelekeza.
Amesema baada ya upekuzi kufanyika wamebaini kuwa bidhaa hizo zenye thamani ya Mamilioni ya shilingi zilingizwa nchini bila kulipiwa kodi mbalimbali za Serikali.
Kwa sababu hiyo meneja huyo wa TRA mkoa wa Mara amesema hivi sasa gari hilo na bidhaa zote zimehifadhiwa katika ofisi ya TRA wilayani Serengeti na kuwataka wamiliki wa gari na bidhaa hizo kujitokeza kulipa kodi hiyo kabla ya hatua nyingine za sheria kuchukuliwa dhidi yao.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment